Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili yaondoa watumishi wazembe Kibaha

Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili yaondoa watumishi wazembe Kibaha - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili yaondoa watumishi wazembe Kibaha, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili yaondoa watumishi wazembe Kibaha
kiungo : Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili yaondoa watumishi wazembe Kibaha

soma pia


Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili yaondoa watumishi wazembe Kibaha

                        Na Frank Mvungi- MAELEZO
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina ameagiza Kuondolewa mara moja kwa watumishi wa Wanaosimamia Kituo cha Ukaguzi Kibaha Mkoani Pwani kwa kushindwa kusimamia rasilimali za Sekta ya Mifugo na Uvuvi. Akizungumza leo Jijini Dodoma wakati  wa kikao cha Tathmini ya Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili iliyofanyika  kati ya mwezi Oktoba na Novemba 2018 ikilenga Kuinua mchango wa Sekta ya Mifugo katika Pato la Taifa Waziri Mpina amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali yatokanayo na biashara ya Mifugo na Mazao yake.

“ Watumishi wote walioshiriki katika Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili wamefanya kazi kubwa na kwa uzalendo mkubwa hivyo nawapongeza kwa kuwa mmeonesha kuwa tunao uwezo wa kusimamia rasilimali zetu ili zitoe mchango stahiki katika pato la Taifa”.Alisisitiza Mhe. Mpina. Akifafanua amesema watumishi wasio waadilfu na wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao hawana nafasi katika Wizara hiyo ndio maana ameagiza kuondolewa mara moja kwa watumishi wanaofanya kazi ya ukaguzi wa rasilimali hizo katika kituo cha Kibaha.
Aliongeza kuwa Operesheni Nzagamba awamu ya Pili, 2018 imedhihirisha kwamba usimamizi thabiti wa Sheria, Kanuni na Taratibu katika Sekta ya Mifugo unaweza kuleta tija kwa kuongeza uzalishaji bora wa mazao ya mifugo ambayo ni malighafi ya Viwanda na hivyo kuchangia ipasavyo katika kuendeleza uchumi wa Viwanda.

“ Ni mategemeo yangu kuwa wananchi mtakuwa wazalendo kwa nchi yetu kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Kufanya biashara ya mifugo pia kutoa taarifa pale mnapobaini utoroshaji wa mifugo kwenda nchi jirani bila kulipiwa ushuru na tozo stahiki ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya watu hao”. Alibainisha Mhe. Mpina. Pia aliwaasa Watumishi wa Wizara hiyo na wale wa Halmashauri kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa makini utekelezaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu zote zinazosimamia biashara ya Mifugo na Mazao yake hususan mabadiliko ya Kanuni mpya iliyotolewa mwezi Agosti, 2018.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya Tathmini ya Matokeo ya Operesheni Nzagamba awamu ya pili leo Jijini Dodoma.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa Taarifa ya Tathmini ya Matokeo ya Operesheni Nzagamba awamu ya pili  katika ukumbi wa St.Gasper Leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina akifuatilia uwasilishwaji wa Taarifa ya Tathmini ya Matokeo ya Operesheni Nzagamba awamu ya pili  leo Jijini Dodoma.Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel,Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo.     
 Baadhi ya Maafisa wa Polisi walioshiriki  Operesheni Nzagamba awamu ya pili  wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luhaga Mpina (hayupo)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA     


Hivyo makala Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili yaondoa watumishi wazembe Kibaha

yaani makala yote Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili yaondoa watumishi wazembe Kibaha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili yaondoa watumishi wazembe Kibaha mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/operesheni-nzagamba-awamu-ya-pili.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Operesheni Nzagamba Awamu ya Pili yaondoa watumishi wazembe Kibaha"

Post a Comment