Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara

Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara
kiungo : Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara

soma pia


Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara

Mkutano kati ya Tanzania na Uganda kujadili namna ya kuimairisha mahusiano ya kibiashara na kiuchumi ulifanyika Mutukula, Uganda kuanzia tarehe 17 hadi 19 Desemba 2018. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde waliongoza ujumbe wa nchi zao katika mkutano huo.

Mkutano huo ulihitimishwa kwa Mawaziri kusaini taarifa ya makubaliano ambayo pamoja na mambo mengine, waliafikiana kuvitafutia ufumbuzi vikwazo vya kibishara na vile visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha biashara baina ya nchi hizo mbili.

Mkutano huo ulianza kwa ngazi ya Wataalamu na Makatibu Wakuu ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph R. Buchwaishaija.

Aidha, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz Ponary Mlima na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Mhe. Richard Kabonero walishiriki mkutano huo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mutukula, Uganda
20 Desemba 2018
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Joseph Kakunda (kulia) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Ushirika wa Uganda, Mhe. Amelia Kyabambadde wakibadilishana taarifa ya mkutano kati ya Tanzania na Uganda uliojadili namna ya kuimarisha biashara na kuondoa vikwazo vya kibiashara na visivyokuwa vya kiforodha uliofanyika Mutukula, Uganda tarehe 19 Desemba 2018.


Hivyo makala Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara

yaani makala yote Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/tanzania-na-uganda-zakubaliana.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Tanzania na Uganda zakubaliana kuimarisha Biashara"

Post a Comment