NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA
kiungo : NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

soma pia


NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA


LUSUNGU HELELA-GEITA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amesali katika Kanisa la Wasabato la Geita Kati mkoani Geita ambako ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha Afya.

Lengo la kuendesha harambee hiyo ni kwa ajili ya kuchangisha pesa zitakazotumika katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kanisa la Wasabato kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo kitakachosaidia kuihudumia jamii.

Katika harambee hiyo Naibu Waziri Mhe. Kanyasu aliambatana na wadau wake ambapo kwa pamoja waliweza kukabidhi Sh15 milioni zikiwa ni fedha taslimu kama mchango wao.Katika harambee hiyo, ahadi mbali mbali zimeweza kutolewa ikiwemo matofali, saruji pamoja na malori ya mchanga na mawe.

Sambamba na hilo, Mhe. Kanyasu ameupongeza uongozi wa kanisa hilo kwa kuwa na mpango huo wa kuisaidia serikali katika kutoa huduma kwa jamii ambayo kimsingi ni kazi ya Serikali,”Suala la kujenga vituo vya afya ni jukumu la serikali lakini ninyi mmeamua kuisaidia serikali nawapongezeni sana na msisite kunishirikisha kwa lolote.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( wa pili kushoto) akizungumza mara baada ya ibada iliyofanyika katika ya Kanisa la Wasabato la Geita kati wakati ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita

Baadhi ya waumini ibada wa Kanisa la Wasabato la Geita kati wakifuatilia ibada kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa  kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita.

Mchungaji na Mwenyekiti wa South Nyanza Conference, Sadoki Butoke akitoa mahubiri kwa waumini waliojumuika katika ibada ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu (katikati) akiwa na baadhi ya watendaji wa mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Kanisa la Wasabato la Geita wakisikiliza mahubiri kabla ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo afya kinachotarajiwa kujengwa katika kata ya Bombambili eneo la Magogo mkoani Geita. 




Hivyo makala NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

yaani makala yote NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/naibu-waziri-kanyasu-aendesha-harambee.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU WAZIRI KANYASU AENDESHA HARAMBEE KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA"

Post a Comment