PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA.

PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA.
kiungo : PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA.

soma pia


PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA.

SHIRIKA la ndege la Kitanzania Precision Air limedhamiria kuanzisha safari za kwenda Chato na makao makuu ya nchi mkoani Dodoma. Shirika hilo lenye miaka 25 tangia kuanzishwa kwake kwa sasa linafanya safari za ndani zipatazo kumi. 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Meneja Masoko na Mawasiliano Hillary Mremi amesema, Precision Air imegundua kuna fursa ya kutanua soko lake kupitia safari hizo za Chato na Dodoma na kwamba tayari wameshaanza mchakato wa kutathimini masoko hayo ili kuandaa safari zitakazo kidhi mahitaji ya maeneo hayo. 

“Kumekuwa na matukio muhimu katika maeneo haya, kwa upande mmoja na  hatua ya Serekali kuhamia Dodoma ni dhahiri itaongeza safari za watu kwenda na kutoka Dodoma. Precision Air kama shirika linalongoza kwa kuwa na mtandao bora wa safari na Shirika pekee la Ndege ambalo ni mwanachama wa IATA nchini Tanzania tumedhamiria kuanzisha safari za Dodoma ili kuwawezesha wateja wetu wanosafiri kupitia mtandao wetu mpana wa safari kuunganisha safari zao kwenda Dodoma," ameeleza Mremi. 

Akiongelea dhamira ya Precision Air kuanzisha safari za Chato, Mremi amesema ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Chato umefungua milango kwa Precision Air kujitanua zaidi katika ukanda wa Ziwa.  Huku safari za Chato zitalenga kuhudumia mkoa wa Geita ambao una shughuli mbali mbali za kiuchumi ikiwa ni pamoja na Uchimbaji wa madini, Uvuvi na Utalii.

“Tunapenda kuipongeza serekali yetu kwa jitihada zake za za kuboresha viwanja vyetu vya ndege, jambo ambalo litatuwezesha sisi watoa huduma kuanzisha safari nyingi zaidi ambazo zitaifungua nchi na kuongeza kasi ya maendeleo. Mipango yetu ni kuanzisha safari zetu za Chato na Dodoma katika majira ya joto mwaka 2019," amefafanua Bw.Mremi. 

Precision Air ilianzishwa mnamo mwaka 1993 kama shirika binafsi la ndege za kukodi,Shirika la ndege la Precision Air limeendelea kukua na kuwa moja ya mashirika ya ndege ya nayoheshimika Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.Kwa sasa Shirika hilo linafanya safari za ndani na nje kuelekea sehemu takribani 11. Ikitokea Dar es Salaam (makao makuu) Precision Air inasafiri kuelekea Arusha, Bukoba, Kahama, Kilimanjaro, Musoma, Mtwara, Mwanza, Tabora, Zanzibar, Seronera,Nairobi na Entebbe


Hivyo makala PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA.

yaani makala yote PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/precision-air-yadhamiria-kuanza-safari.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "PRECISION AIR YADHAMIRIA KUANZA SAFARI ZA CHATO NA DODOMA."

Post a Comment