title : NAIBU MEYA ILALA AMEKULA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA WAJANE ,ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII.
kiungo : NAIBU MEYA ILALA AMEKULA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA WAJANE ,ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII.
NAIBU MEYA ILALA AMEKULA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA WAJANE ,ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII.
Na. John Luhende
Mwamba wa habari
Akina Mama wajane katika kata ya vingunguti wametakiwa kuwa na umoja ili kuwa kukabili changamoto za maisha zinazowakabili na kuweza kupata msaada wa kijamii kutoka serikalini na wafadhili mbalimbali na watu binafsi .
Wito huo umetolewa na Naibu meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Vingumguti Omary Kumbilamoto, alipokuwa akitoa msaada wa vyakula kwaajili ya sikuu ya Christmas kwa kikundi cha Upendo cha akinamama wajane kata ya Vinguti , na kuitaka jamii kutoyasahau makundi ya wajane yatima na walemavu.
‘’Akina Mama hawa hawakuwa na pakushika sikukuu hii, ni likutana nao siku tatu zilizopita wakaniomba nikawaahidi kuwa saidia, na leo nimewaletea Mchele kilo 100,na Mafuta ndoo moja , kubwa zaidi nina sisitiza wawe na umoja ili iwe rahisi kuwa fikia na kuwapa msaada,namimi nimefanya mengi katika kata hii ikiwemo kununua gari la wagnjwa katika zahanati ya Vingunguti, nitawasaidia kuwa tafutia wadu na pia nitamleta afisa Maendeleo ili awape elimu na wafungue account “alisema
Aidha Kumbilamoto ameitaka jamii kuwa na huruma kwa wajane kutowanyang’anya mali walizo achiwa na waumezao.
“Naomba jamii tuyaangalie haya makundi maalum ya Walemavu wajane na Yatima ,pia sibusara sana kwa wanajamii kunnyang’anya maliza za malehemu wajane wanateseka na yatima, kwa hapa Vingunguti tuna viwanda 41, nita waomba nao wasaidie kundi hili “alisema
Kwa upande wake mwalimmu wa kikundi hicho Jane Raulent, amesema amefanikiwa kuwaweka pamoja wajane hao na sasa wana saidiana kuweza kupata chakula kwa kuchangia fedha kidogo.
‘’Nimejaribu kuwa saidia kwa kuwaweka pamoja hapa mwanzo walikuwa wanateseka walikuwa wanaokota vikuni na vifuu barabarani na chakula ilikuwa shida kwa sasa wanachangiana chakula kwa kuto shilingi elfu tano kila mjane anapata kiroba kimoja cha unga , na muda mwingine mafuta ya taa na mkaa”alisema
Nao baa dhi ya akimama wajane waliopatafursa ya kuzungumza wamemshukuru Naibu Meye Kumbilamoto kwa msaada aliowapa na kumuoma awatafutie wafadili wa kikundi hicho.
“Jinalangu naitwa Mariam Daud Hashim,ni mjane nifiwa na Mume wangu 2007, haijawahitokea kwa viongozi hatawaliopita sikuwahi kuwaona wakisaidia wajane hadi mimi leo nimetimiza miaka 70, naona viongozi waliowengi wanajali familia zao na wanajilimbikizia mali , tunakushukuru wewe Baba kwa moyo wakutoa Mwenyezi Mungu akuzidishie ulipotoa ’’alisema.
Hivyo makala NAIBU MEYA ILALA AMEKULA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA WAJANE ,ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII.
yaani makala yote NAIBU MEYA ILALA AMEKULA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA WAJANE ,ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU MEYA ILALA AMEKULA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA WAJANE ,ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/naibu-meya-ilala-amekula-sikukuu-ya.html
0 Response to "NAIBU MEYA ILALA AMEKULA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA WAJANE ,ATOA UJUMBE MZITO KWA JAMII."
Post a Comment