title : WAZIRI KALEMANI AAGIZA WOTE WALIOLIPIA UMEME 2017 WAUNGANISHIWE KABLA YA MWISHO WA MWAKA
kiungo : WAZIRI KALEMANI AAGIZA WOTE WALIOLIPIA UMEME 2017 WAUNGANISHIWE KABLA YA MWISHO WA MWAKA
WAZIRI KALEMANI AAGIZA WOTE WALIOLIPIA UMEME 2017 WAUNGANISHIWE KABLA YA MWISHO WA MWAKA
Na Veronica Simba .
Serikali imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhakikisha wateja wote walioomba na kulipia huduma hiyo mwaka 2017 wanaunganishiwa kabla ya Desemba 30 mwaka huu.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alitoa agizo hilo kwa nyakati tofauti hivi karibuni, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme mkoani Singida na Dodoma.“Agizo hili ni kwa nchi nzima. Hakikisheni wateja waliowasilisha maombi yao na kulipia ndani ya mwaka huu wa 2017 wawe wameunganishiwa umeme siyo zaidi ya Desemba 30 mwaka huu.”.
Aidha, Dkt Kalemani aliwaagiza watendaji wa shirika hilo kutoa elimu kwa umma, hasa wananchi walioko vijijini kuhusu umuhimu wa kutumia umeme ili kuwahamasisha kuunganisha nishati hiyo katika makazi yao.
Akifafanua, Waziri alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa baadhi ya wananchi hawajaunganisha umeme katika makazi yao japokuwa tayari Serikali imekwishawafikishia nishati hiyo katika maeneo yao.“Inawezekana baadhi ya wananchi hawajatambua umuhimu wa kutumia umeme, hivyo ni vema wapatiwe elimu husika. Tuwatembelee mahali waliko, hususan vijijini na tuwapatie elimu hiyo,” alisisitiza.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ibaga, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, wakati wa ziara yake hivi karibuni kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
Mbunge wa Iramba Mashariki, Allan Kiula akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani jimboni kwake hivi karibuni, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde (kushoto), akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, jimboni kwake hivi karibuni kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Innocent Lupenza, akiandika majina ya baadhi ya wazee waliopatiwa zawadi ya kifaa kijulikanacho kama Umeme Tayari (UMETA) na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa katika ziara ya kazi Mikoa ya Singida na Dodoma hivi karibuni.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI KALEMANI AAGIZA WOTE WALIOLIPIA UMEME 2017 WAUNGANISHIWE KABLA YA MWISHO WA MWAKA
yaani makala yote WAZIRI KALEMANI AAGIZA WOTE WALIOLIPIA UMEME 2017 WAUNGANISHIWE KABLA YA MWISHO WA MWAKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KALEMANI AAGIZA WOTE WALIOLIPIA UMEME 2017 WAUNGANISHIWE KABLA YA MWISHO WA MWAKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/waziri-kalemani-aagiza-wote-waliolipia.html
0 Response to "WAZIRI KALEMANI AAGIZA WOTE WALIOLIPIA UMEME 2017 WAUNGANISHIWE KABLA YA MWISHO WA MWAKA"
Post a Comment