title : MADEREVA WAZEMBE JESHI LA POLISI HALITAWAFUMBIA MACHO
kiungo : MADEREVA WAZEMBE JESHI LA POLISI HALITAWAFUMBIA MACHO
MADEREVA WAZEMBE JESHI LA POLISI HALITAWAFUMBIA MACHO
Na. Vero Ignatus, Arusha
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Fortunatus Musilimu amewaomba abiria kulisadia jeshi la polisi kwa kutoa taarifa pale wanapoona dereva amekaidi sheria ya usalama barabarani, wasisubirie hadi ajali itokee ndipo waanze kutoa malalamiko
Hayo ameyasema leo Jijini alipokuwa akifanya ukaguzi wa magari pamoja na askari wa usalama barabarani na wadau wengine wa usalama katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani ambapo aliwataka abiria kutokufumbia macho uzembe wowote atakaoufanya dereva wa kuhatarisha maisha ya abiria awapo safarini.
Aidha ameeaagiza abiria hao punde wanapomuona dereva anaotaka kulipita gari lingine kimakosa, mwendo kasi, lugha chafu kwa abiria, kuongea na simu sambamba na viashiria vyote vinavyoweza kupelekea kutokea ajali watoe taarifa kwa namba 0656111444
'' Piga simu muda wowote tunapambana sisi tunapambana na madereva wazembe hadi kuhakikisha tunakuwa salama barabarani "'' Tunapozungumzia maisha ya watu hatuna mchezo wacheni uzembe na mambo ya kitotokitoto muwapo barabarani dereva unakimbia kwenda wapi gari limejaa udereva ni taaluma, zingatia sheria uwapo barabarani"alisema Muslimu
Muslim ametahadharisha madereva ambao hawatazingatia na kutii sheria za usalama barabarani kuwa jeshi la polisi halitawafumbia macho sheria itafuata mkondo wake. Pia amesisitiza kuwa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani lipo tayari kwaajili ya waananchi na kuhakikisha usalama wa maisha yao wawapo safarini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Baraka Msangi amesema zoezi la Abiria paza sauti sambamba na ile ya Nyakua ya jeshi la polisi imesababisha ajali zimepungua katika Jiji la Arusha
Amewataka Madereva kuendelea kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani kwasababu abiria wanawategemea wao wawapo safarini
Wa Pili kutoka kulia ni Kamanda wa kikosi cha uslama. Barabarani SACP Fortunatus Musilim, akifuatiwa na Mrakibu msaidizi Joseph Bukombe mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani Arusha, Mjumbe wa Baraza la usalama barabarani Taifa Hamza Kasongo na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani mkoa wa Arusha Bakari Msangi wakiwa stendi kuu leo asubuhi. Picha na Vero Ignatus.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchi SACP Fortunatus Musilimu akizungumza na abiria leo asubuhi katika stendi ya mabasi Jijini Arusha kabla hawajaanza safari. Picha na Vero Ignatus
Baadhi ya mabalozi wa usalama barabarani wakiwa tayari kwa kupaza sauti stendi kuu ya mabasi jijini Arusha. 

Kutoka kulia ni Kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani SACP Fortunatus Musilim ni mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Jijini Arusha Joseph Bukombe, Mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Bakari Msangi. Picha na Vero Ignatus.
Hivyo makala MADEREVA WAZEMBE JESHI LA POLISI HALITAWAFUMBIA MACHO
yaani makala yote MADEREVA WAZEMBE JESHI LA POLISI HALITAWAFUMBIA MACHO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MADEREVA WAZEMBE JESHI LA POLISI HALITAWAFUMBIA MACHO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/madereva-wazembe-jeshi-la-polisi.html
0 Response to "MADEREVA WAZEMBE JESHI LA POLISI HALITAWAFUMBIA MACHO"
Post a Comment