KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA

KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA
kiungo : KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA

soma pia


KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ametaka kero ya maji kwa wakazi wa Mtoni itatuliwe haraka iwezekanavyo mara baada kujionea hali huduma ya maji kwa wananchi. 

Amezungumza hayo katika muendelezo wa ziara yake ya kusiskiliza kero za wananchi jijini Dar es Salaam, na kuitaka DAWASA itafute suluhisho la kufikisha huduma ya maji kwa wananchi, ukizingatia uwepo wa chanzo cha maji na mtambo wa kusafishia maji katika eneo la Mtoni.

Profesa Mbarawa amesema haoni sababu ya wananchi hao kukosa maji kwa kuwa kuna chanzo cha maji cha uhakika, kinachohitajika ni kuweka mkakati mzuri wa ujenzi wa miundombinu itakayofikisha maji kwa wananchi kwa kuwa chanzo kipo. Akiwa kwenye Mtaa wa Mashine ya Maji, Profesa Mbarawa amekutana na kero ya maji kutoka kwa wananchi ambao wamesema maji wanayotumia yanayotoka kwenye kisima usalama wake ni mdogo, kumuomba Waziri wa Maji awatatulie changamoto hiyo.

Aidha, wamemuomba Waziri wa Maji aipatie ufumbuzi changamoto ya kisima kilichochimbwa na Halmashauri ya Temeke kilichokuwa kikitumika awali kwa ajili ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi kuhodhiwa na mtu binafsi wakati wao wakiwa na uhitaji mkubwa wa maji. Akijibu hoja za wananchi hao Profesa Mbarawa amesema atatuma timu ya wataalamu wa DAWASA ifike eneo hilo Jumatatu ijayo, ili waweze kufuatilia jambo hilo kabla ya kuchukua hatua zinazostahili. Pia, waangalie namna jinsi watakavyoweza kufanikisha zoezi la kufikisha huduma ya maji kwa wakazi hao.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku tano katika Jiji la Dar es Salaam; ambapo ametembelea maeneo yenye changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji ya Kimara, Bonyokwa, Salasala na Mtoni kusikiliza kero za wananchi ambazo amekuwa akizisikia kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi. Pamoja na Kiwalani ambapo alikwenda kupata mrejesho kutoka wa wananchi kuhusu maendeleo ya Mradi wa Maji Kiwalani uliozinduliwa hivi karibuni.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akijibu hoja za wananchi mara baada ya kusikiliza kero zao eneo la Mtoni, katika Wilaya ya Temeke. 
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Mtoni, Wilaya ya Temeke wakati akielezea kero yake kuhusu maji. 


Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Meneja wa Mtambo wa Maji Mtoni, Mhandisi Deusdedit Rwegasila alipokuwa ziarani katika eneo la Mtoni, wilayani Temeke. 
Fundi Sanifu Mwandamizi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Robert Chenge akitoa maelezo kuhusu hali ya huduma ya maji kwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa alipokuwa eneo la Mtoni.


Hivyo makala KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA

yaani makala yote KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/kero-ya-mazi-kwa-wakazi-wa-mtoni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KERO YA MAZI KWA WAKAZI WA MTONI ITATULIWE HARAKA-WAZIRI MBARAWA"

Post a Comment