title : KAMATI MAALUM YA NEC Z'BAR YAIPONGEZA SMZ
kiungo : KAMATI MAALUM YA NEC Z'BAR YAIPONGEZA SMZ
KAMATI MAALUM YA NEC Z'BAR YAIPONGEZA SMZ
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
KAMATI Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar imekutana chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, imeunga mkono juhudi za Serikali kusaini Makubaliano ya Mgawanyo wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA) na Kampuni ya RAKGAS ya Ras al Khaimah ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Akitoa ufafanuzi jana Disemba 11, mwaka 2018 juu ya masuala mbali mbali yaliyoazimiwa kupitia Kikao hicho Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi', huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, ameeleza kwamba Kikao hicho kimeipongeza Serikali kwa kusaini mkataba huo na kueleza kuwa ulifuata taratibu zote za kisheria.
Dk. Mabodi aliongeza kwamba maamuzi ya kusaini mkataba huo yametokana na kukamilika kwa taratibu mbali mbali za kisheria kwa pande zote za Muungano ambapo kupitia maamuzi ya kisheria Zanzibar imepewa mamlaka ya kuchimba na kusimamia yenyewe masuala ya Mafuta na Gesi.
Alisema kuwa kufanikiwa kwa mchakato huo wa kusainiwa mkataba huo ni hatua kubwa ya maendeleo iliyofanywa na Dk.Ali Mohamed Shein, kwa kushirikiana na Viongozi mbali mbali wakiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jonh Pombe Magufuli.
WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakiwa katika Kikao cha kawaida kinachofanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, huko Kisiwandui Afisi Kuu Zanzibar.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala KAMATI MAALUM YA NEC Z'BAR YAIPONGEZA SMZ
yaani makala yote KAMATI MAALUM YA NEC Z'BAR YAIPONGEZA SMZ Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI MAALUM YA NEC Z'BAR YAIPONGEZA SMZ mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/kamati-maalum-ya-nec-zbar-yaipongeza-smz.html
0 Response to "KAMATI MAALUM YA NEC Z'BAR YAIPONGEZA SMZ"
Post a Comment