title : SHEKH MKUU DSM ATOA NENO LA KUNUSURU UPINZANI
kiungo : SHEKH MKUU DSM ATOA NENO LA KUNUSURU UPINZANI
SHEKH MKUU DSM ATOA NENO LA KUNUSURU UPINZANI
Mwambawahabari
Na. John Luhende
Shekh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum, amemtaka Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto kuendelea kutumika katika chama chake cha Wananchi CUF ili kuwatia moyo wananchi waliomchagua.
Akizungumza kwa niaba ya Mufti mkuu wa Tanzania Shekh Alhadi amesema kumekuwa na kawaida ya chama cha Mapinduzi CCM, kuwachukua wanasiasa wanaofanya vizuri katika jamii ili waweze kuwa Wana CCM.
"Ndugu Naibu Meya pole Sana kwa msiba uliokupata ila na kuomba jambo moja tulikuwa huko uliko usiache wenzako wamekupigania Sana kupata kiti hicho utakuwa umewavunja moyo huenda CCM wanameshaanza kukuvuta tafadhili tulia na wenzako" Alisema Shekh Alhadi.
Kauli hiyo imekuja baada siku za hivi karibuni wanasiasa wa vya vya upinzani kuvihama vyama vyao na kujiunga naChama cha Mapinduzi CCM jambo ambao limeleta s into fahamu kuhusu uhai wa vyama vya upinzani nchini.
Msiba huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa, akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Sophia Mjema , madiwani wa Manispaa ya Ilala ndugu Jamaa na marafiki kutoka ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam, na marehemu atasafirishwa kwenda Kisarawe kijiji cha Kauzeni mkoani Pwani kwa ajili ya maziko.
Hivyo makala SHEKH MKUU DSM ATOA NENO LA KUNUSURU UPINZANI
yaani makala yote SHEKH MKUU DSM ATOA NENO LA KUNUSURU UPINZANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHEKH MKUU DSM ATOA NENO LA KUNUSURU UPINZANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/shekh-mkuu-dsm-atoa-neno-la-kunusuru.html
0 Response to "SHEKH MKUU DSM ATOA NENO LA KUNUSURU UPINZANI"
Post a Comment