title : MBOWE, VIGOGO WENZAKE CHADEMA WATOKA MAHABUSU KWA DHAMANA
kiungo : MBOWE, VIGOGO WENZAKE CHADEMA WATOKA MAHABUSU KWA DHAMANA
MBOWE, VIGOGO WENZAKE CHADEMA WATOKA MAHABUSU KWA DHAMANA
Na Bakari Majeshi, Globu ya jamii
HATIMAYE baada ya kukaa mahabusu kwa siku saba na kusherehekea sikuu ya Pasaka wakiwa gerezani,Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe pamoja na vigogo wengine sita wa chama hicho leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana,baada ya kukamilisha masharti ya dhamana.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka tisa yakiwemo ya Uchochezi wa Uasi na kufanya mkusanyiko isivyo halali kinyume cha sheria.
Mbali ya Mbowe washtakiwa wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu Bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.
Wengine ni Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko na Katibu wa chama hicho Dk .Vicenti Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima Mdee ambaye ameunganishwa na wenzake hao leo.
Mdee alikamatwa Jumapili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Afrika Kusini.
Akisoma masharti ya dhamana, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amewataka washtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh.milioni 20 kila mmoja.
Pia wadhamini hao wametakiwa kuwa na barua za utambulisho zinazoamika na vitambulisho huku pia wakitakiwa kuripoti katika kituo kikuu cha polisi cha kati kwa mkuu wa polisi mara moja kwa wiki siku ya Ijumaa.
Mapema, kabla ya kusomewa masharti ya dhamana, washtakiwa walisomewa upya mashtaka yao baada wa Wakili wa Serikali Faraja Nchimbi kumuongeza Mdee katika kesi hiyo na kufanya idadi ya mashtaka kufikia tisa na washtakiwa saba.
Akisoma mashtaka hayo, Nchimbi amedai Februari 16, mwaka huu katika barabara ya Kawawa Mkwajuni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, walifanya mkusanyiko usio halali kinyume na sheria wakiwa na nia ya kutekeleza lengo la pamoja na kufanya watu waogope kwamba watakwenda kusababisha uvunjifu wa amani.
Aidha Nchimbi amedai Februari 16, mwaka huu katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni, washtakiwa wakiwa wamekusanyika wao na wenzao 12 ambao bado hawajafikishwa mahakamani, wakiwa kwenye maandamano hayo,licha ya kutolewa tamko la kuwataka kutawanyika...waligoma kutii amri hiyo na kuendelea na maandamano na kusababisha kifo cha Aquilina Akwkilina kusababisha askari wawili kujeruhiwa kutokana na mkusanyiko huo.
Katika shtaka la tatu imedaiwa Februari 16, mwaka huu katika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, jijini mshtakiwa Mbowe peke yake wakati akihutubia wananchi wa jimbo hilo alihamasisha chuki isivyohalali kwa kutoa matamshi ya kuhamasisha chuki maneno yaliyosababisha chuki mioyoni mwa wana jamii.
Pia Mbowe anadaiwa kufanya uchochezi na kusababisha chuki miongoni mwa wanajamii ya watanzania kinyume na sheria.
Aidha Nchimbi amedai katika mashitaka ya uchochezi wa uasi yanayomkabili Mbowe, inadaiwa akiwa maeneo hayo katika mkutano wa hadhara, akiwa na nia ya kupandikiza chuki na dharau kwa watanzania dhidi ya uongozi wa kiserikali uliopo madarakani kisheria,
Imedaiwa alitamka maneno yenye kupandikiza chuki na kuleta ushawishi wa uasi dhidi ya serikali iliyopo madarakani kisheria
Nchimbi aliendelea kudai, katika tarehe hiyo hiyo na maeneo hayo mkoani Dar es Salaam, Mbowe alitoa matamshi ya kupandikiza chuki na dharau dhidi ya mamlaka halali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Katika shitaka la saba, Mbowe anakabiliwa na tuhuma za kutenda kosa la kushawishi kutendeka kwa kosa la jinai, ambapo amedaiwa siku hiyo, akiwa pia amejumuika na wengine ambao hawako mahakamani, aliwashawishi wakazi hao wa Kinondoni, kutenda kosa la kufanya maandamano na mkusanyiko usio wa halali.
Mshtakia Msigwa anadaiwa kushawishi raia kutenda kosa la jinai shtaka analodaiwa kutenda Februari 16, mwaka huu katika maeneo hayo hayo ya Viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni Dar es Salaam,
Imedaiwa siku hiyo Msigwa aliwashawishi wananchi wa Kinondoni kutembea mbele ya umma wakiwa na silaha.
Katika shtaka linalomkabili Mdee, imedaiwa Februari 16 mwaka ,2018 katika viwanja vya Buibui vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaam akiwa anahutubia wananchi na wakazi wa eneo hilo alitoa matamshi yafuatayo "Sitaki kusimulia madhila yanayomkumba kila mtu katika Serikali ya awamu ya tano, tunaomba tukamchinje Magufuli na vibaraka wake wote kama mbwai na iwe mbwai,"..
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 16 mwaka 2018 kwa ajili ya washtakiwa kuja kusomewa Maelezo ya awali (PH).
Hivyo makala MBOWE, VIGOGO WENZAKE CHADEMA WATOKA MAHABUSU KWA DHAMANA
yaani makala yote MBOWE, VIGOGO WENZAKE CHADEMA WATOKA MAHABUSU KWA DHAMANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBOWE, VIGOGO WENZAKE CHADEMA WATOKA MAHABUSU KWA DHAMANA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/mbowe-vigogo-wenzake-chadema-watoka.html
0 Response to "MBOWE, VIGOGO WENZAKE CHADEMA WATOKA MAHABUSU KWA DHAMANA"
Post a Comment