DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR

DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR
kiungo : DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR

soma pia


DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi, amesema CCM imendelea kusimamia kwa ufanisi sera za maendeleo kwa jamii bila kujali itikadi za kisiasa. Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Watendaji wa Baraza la Manispaa Mjini, huko Sebleni katika mwendelezo wa ziara yakeb ya kukagua miradi mbali mbali iliyotekelezwa na manispaa chini ya mfumo wa Ugatuzi.

Dk.Mabodi ameeleza kwamba mipango endelevu inayotekezwa na Serikali za mitaa kwa lengo la kuimarisha huduma muhimu za kijamii katika nyanja za afya,elimu,uvuvi,ufugaji,kilimo na ujasiriamali ni kwa ajili ya wananchi wa rika zote bila ya kubaguliwa. Ameeleza kuwa Serikali Kuu imeamua kupeleka madaraka katika Serikali za Mitaa kwa lengo kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za kijamii kwa wananchi.

Ameeleza kwamba utekelezaji mzuri wa mipango iliyomo katika ugatuzi ndio litakuwa ni chimbuko la utengenezwaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025, iliyokuwa bora na inayoendana mahitaji halisi ya wananchi. Pamoja na hayo amewasihi Watendaji wote waliotolewa Serikali Kuu na kupelekwa Serikali za mitaa kuendelea kuwa wazalendo wenye kujituma kwa moyo mmoja katika kuhudumia jamii.

Kupitia ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo, aliitaka Manispaa hiyo kuhakikisha miradi mbali mbali inayotelezwa inakuwa ndio vipaumbele halisi vya wananchi husika katika maeneo yao na inakuwa na viwango vinavyokubalika kisheria.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi  akielekea  katika ukaguzi wa ujenzi wa jengo la kisasa la machinjio ya kuku katika Soko la Darajani.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akipokea maelezo juu ya maendeo yaliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la soko la kuku darajani.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akikagua shamba la mboga mboga la kikundi cha shehia ya Nyerere iliyopo katika Wadi ya Amani ambao wanajishughulisha na kilimo na wanasaidiwa na Manispaa ya Majini katika kazi zao.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Afisa  Muunguzi  Ashura Amour Mwinyi (kulia)  wa Kituo cha Mamama  Wajawazito na Watoto cha Sebleni akielezea huduma za Afya zinazotolewa bure katika kituo hicho zikiwemo za kipimo cha Ultra Sound.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akipewa maelezo ya mashine maalum ya kusaga taka taka za kutengenezea mbolea ya mimea huko katika kikundi cha ujasiriamali kilichopo Shauri Moyo Zanzibar , katika ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na Manispaa ya Mjini chini ya ugatuzi.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR

yaani makala yote DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/dkt-mabodi-afanya-ziara-manispaa-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR"

Post a Comment