title : JUKWAA LA USIMAMIZI WA MAAFA LAHITAJI UTASHI KISIASA,KISHERIA -PROF KAMUZORA
kiungo : JUKWAA LA USIMAMIZI WA MAAFA LAHITAJI UTASHI KISIASA,KISHERIA -PROF KAMUZORA
JUKWAA LA USIMAMIZI WA MAAFA LAHITAJI UTASHI KISIASA,KISHERIA -PROF KAMUZORA
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu),Profesa Faustine Kamuzora amesema jukwaa la usimamizi wa maafa la Taifa linahitaji utashi wa kisiasa,uwajibikaji kisheria ,uelewa wa umma ,elimu ya kisayansi na mipango makini ya maendeleo ili kutekeleza majukumu yake.
Profesa Kamuzora amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua jukwaa la Usimamizi wa Maafa la Taifa lililofanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam.
“Jukwaa hili ni chombo cha kisheria hapa nchini kwa ajili ya kutathmini na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali kuhusu majanga ya aina zote, hivyo linaundwa kwa kuzingatia kifungu cha 40 cha Sheria ya Usimamizi wa maafa namba 7 ya mwaka 2015,” amesema Profesa Kamuzora.
Amesema jukwaa hilo linakutana kwa mara ya kwanza toka sharia hiyo ianze kutumika hapa nchini, hivyo jukwaa linatoa fursa ya utaratibu wa usimamizi wa maafa kwa ushirikiano wa wataalam wa fani mbalimbali kwa kujumuisha sekta ya umma na sekta binafsi, mashirika ya kimataifa na Umoja wa Mataifa.
Ameongeza jukwaa linawajibu wa kushughulikia changamoto za kijamii ,kiuchumi na mazingira ya kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufanikisha kujumuisha upunguzaji wa madhara ya maafa katika mipango na sera za maendeleo ya Taifa na katika misaada ya kibinadamu.
Hivyo makala JUKWAA LA USIMAMIZI WA MAAFA LAHITAJI UTASHI KISIASA,KISHERIA -PROF KAMUZORA
yaani makala yote JUKWAA LA USIMAMIZI WA MAAFA LAHITAJI UTASHI KISIASA,KISHERIA -PROF KAMUZORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JUKWAA LA USIMAMIZI WA MAAFA LAHITAJI UTASHI KISIASA,KISHERIA -PROF KAMUZORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/jukwaa-la-usimamizi-wa-maafa-lahitaji.html
0 Response to "JUKWAA LA USIMAMIZI WA MAAFA LAHITAJI UTASHI KISIASA,KISHERIA -PROF KAMUZORA"
Post a Comment