title : BENKI YA I&M KUWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU
kiungo : BENKI YA I&M KUWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU
BENKI YA I&M KUWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU
Na Agness Francis, Globu ya Jamii
Benki ya I & M inaendelea kutoa zawadi kwa wateja wake katika droo ya pili JIDABO na I & M bank chini ya usimamizi kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha iliyochezeshwa leo ambapo washindi watano wamepatikana kutoka sehemu mbali mbali hapa nchini
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Wateja na reja reja, Ndabu Swere amesema kuwa promosheni hiyo iliyoanza mwezi Octoba na kuendelea mpaka Disemba kwa kila mwezi kutaja washindi watano wa droo hiyo.
Ndabu amesema washindi watano waliopatikana leo ni sehemu ya washindi 15 ambao watapatikana katika kipindi chote cha miezi mitatu ya promosheni ya "JIDABO na I&M". Aidha Ndabu amesema kuwa mpaka sasa wameshapata jumla ya washindi 10 na kubakiza wengine 5 ambao watapatikana katika droo ya mwezi huu
"Ili kuweza kushiriki Promosheni hii mteja anapaswa afungue akaunti ya Akiba, biashara, mtoto katika tawi lolote la Benki ya I & M katika kipindi chote cha promosheni, kwa mteja ambaye tayari ana Akaunti ya Benki hiyo anapaswa kuhakikisha kuwa ana akiba ya kiasi cha fedha shilingi 200000, akiwa anamiliki akaunti ya biashara, au 100000, Ikiwa anamiliki Akaunti nyingine zinazohusika katika promosheni," amesema Ndabu.
Mkuu wa kitengo cha Wateja wa reja reja wa Benki ya I & M Ndabu Lilian Swere akiwataja washindi watano wa droo ya pili ya Promosheni ya JIDABO na I& M Bank iliyochezwa leo Jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Mawasiliano Emmanuel Kiondo, Benki ya I & M akiwa na mmoja ya mfanyakazi wa Benki hiyo wakichezesha droo ya pili iliyofanyika leo na kuwatangaza washindi watano wa Promoshei ya JIDABO na I & M Bank chini ya usimamizi kutoka bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha.
Hivyo makala BENKI YA I&M KUWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU
yaani makala yote BENKI YA I&M KUWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YA I&M KUWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/benki-ya-i-kuwaweka-karibu-wateja-wake.html
0 Response to "BENKI YA I&M KUWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE KATIKA MSIMU HUU WA SIKUKUU"
Post a Comment