title : TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA CIIE YATAKAYOFANYIKA SHANGHAI NCHINI CHINA
kiungo : TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA CIIE YATAKAYOFANYIKA SHANGHAI NCHINI CHINA
TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA CIIE YATAKAYOFANYIKA SHANGHAI NCHINI CHINA
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KATIKA kuendeleza mkakati wa kutangaza utalii wa Tanzania nchini China, Bodi ya Utalii Nchini (TTB) kwa kushirikiana na wadau wa Utalii wa Tanzania pamoja na Sekta ya Madini inashiriki onesho kubwa la biashara yaliyoandaliwa na Serikali ya China.
Maonesho hayo makubwa yajulikanayo kama China International Impact Expo (CIIE) yatafanyika katika jiji la Shanghai kuanzia 5-10 Novemba, 2018 na Kupitia maonesho haya, sekta ya madini itaudhihirishia ulimwengu kuwa Madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu.
Akielezea safari hiyo ya nchini China, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema kuwa safari hiyo ya nchini China imeandaliwa na bodi ya utalii kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini China na Shirika la Ndege la Tanzania ATCL, wameandaa ziara ya utangazaji nchini China ambapo pamoja na kushiriki maonyesho ya CIIE watafanya ziara ya utangazaji katika miji mbalimbali.
Amesema miji hiyo ni Shanghai (12 Novemba, 2018), Guangzhou (14 Novemba, 2018), Hong Kong (16 Novemba, 2018), Chengdu (19 Novemba, 2018) na Beijing (20 Novemba, 2018). Misafara hii itatuwezesha kukutana na wafanyabiashara wa utalii wakubwa katika miji hiyo na wawekezaji wakubwa katika sekta ya utalii pamoja na vyombo vya habari mbalimbali vya China.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Jaji Mstaafu Thomas akizungumzia safari ya China na ushiriki wao wa Maonesho makubwa yajulikanayo kama China International Impact Expo (CIIE) yatafanyika katika jiji la Shanghai kuanzia 5-10 Novemba, 2018, Kushoto ni Mihayo Meneja Masoko na Usambazaji Edward Mkwabi.
Hivyo makala TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA CIIE YATAKAYOFANYIKA SHANGHAI NCHINI CHINA
yaani makala yote TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA CIIE YATAKAYOFANYIKA SHANGHAI NCHINI CHINA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA CIIE YATAKAYOFANYIKA SHANGHAI NCHINI CHINA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/tanzania-kushiriki-maonesho-ya-ciie.html
0 Response to "TANZANIA KUSHIRIKI MAONESHO YA CIIE YATAKAYOFANYIKA SHANGHAI NCHINI CHINA"
Post a Comment