title : MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WANAOHALIBU VYANZO VYA MAJI
kiungo : MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WANAOHALIBU VYANZO VYA MAJI
MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WANAOHALIBU VYANZO VYA MAJI
Na David Nyembe, Chunya
MKUU wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Maryprisca Mahundi, amewapa wiki tatu wafugaji wa Kijiji cha Igundu katika Kata ya Sangambi wilayani humo kuhamisha mifugo yao na kuipeleka katika Kijiji cha Paris ambacho kimetengwa kwa ajili ya wafugaji.
Ametoa kauli hiyo wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika kijijini hapo ambapo alisema lengo la kuondoa mifugo hiyo ni kumaliza mgogoro kati ya wakulima wa kijiji hicho na wafugaji pamoja na kuokoa chanzo cha maji ambacho wakazi wa eneo hilo wanakitegemea. Alimuagiza Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Joseph Nangale, kusimamia na kuhakikisha mifugo hiyo inahamishwa huku akimtaka kutumia nguvu iliyotumika kuwazuia wakulima kufanya shughuli zao karibu na chanzo cha maji.
Mahundi alisema amechoshwa na migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijji hicho cha Igundu na kwamba agizo lake hilo ni la mwisho na kwamba atakaporudi tena kwenye kijiji hicho na kukuta inaendelea hakutakuwa na majadiliano tena na kwamba wasije wakamlaumu.
“Mkae chini mjadiliane na mkubaliane idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji wa kijiji hiki atatakiwa kubaki nayo hapa, nimewapa siku 10 viongozi wenu waniletee taarifa ya majidiriano hayo, lakini nimewashauri kila mfugaji abaki na mifugo 10,” alisema Mahundi.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Meryprisca Mahundi (katikati) akimkisikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Kata ya Sangambi kijiji cha Igundu Joseph Nangale ,kuhusiana na namna ambavyo wafugaji wamefanya uhalibifu wa vyanzo vya maji katika kjiji hicho.Picha David Nyembe .
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mh Meryprisca Mahundi (Katikati)akiteta jambo na viongozi wa vijiji vinavyo zunguka kata ya Sangambi ambako kumefanyika uhalibifu wa vyanzo vya maji kutokana na baadhi ya wafugaji wa vijiji hivyo kunywesha mifugo yao sanjali na kupitisha mifugo katika maeneo ya vyazno hivyo.
Wananchi wa kijiji cha Igundu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chunya Merryprisca Mahundi (hayupo pichani) mara baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea maeneo ya vyanzo vya maji ambako kumefanyika uhalibifu mkubwa kutokana na baadhi ya wafugaji kupitisha mifugo yao .
Hivyo makala MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WANAOHALIBU VYANZO VYA MAJI
yaani makala yote MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WANAOHALIBU VYANZO VYA MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WANAOHALIBU VYANZO VYA MAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mkuu-wa-wilaya-ya-chunya-aahidi.html
0 Response to "MKUU WA WILAYA YA CHUNYA AAHIDI KUPAMBANA NA WAFUGAJI WANAOHALIBU VYANZO VYA MAJI"
Post a Comment