- Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa , tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title :
kiungo :

soma pia


Na Judith Mhina -MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amewaapisha wateule aliiowateua hivi karibuni katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri  katika Wizara za  Kilimo  na Ushirika pamoja na Viwanda na Biashara .

Mawaziri walioapishwa ni  Japhet Hasungwa kuwa Waziri wa Kilimo na Ushirika ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,  na Joseph  Kakunda kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Akiongea mara baada ya kuawaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri wanne Rais Magufuli amesema “Korosho sasa itanunuliwa na serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania –TADB kwa shilingi 3300 kwa kilo”

Rais Magufuli ameelezea sababu za kufanya mabadiliko hayo ni kutokana na sekta hizo mbili kutopiga hatua na kuendana na kasi ya serikali yake ya kuinua hali za maisha za wakulima badala yake kuwanufaisha wajanja wachache.

Rais Magufuli amesema mfano ni kasoro zilizojitokeza mpaka kupatiwa ufumbuzi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati wa ziara yake Mkoa wa Kagera. Wakulima wa Kahawa wanalalamikia bei ya Kahawa Bodi inawaambia mpaka ikapange bei Moshi matokeo yake baadhi ya watumishi kushiriki katika biashara ya magendo na nchi jirani kwa kujinufaisha wao binafsi na kuwaacha wakulima bila msaada

Aidha Rais Magufuli ameonyesha udhaifu wa Wizara ya kilimo katika kusimamia zao la Korosho ambapo amesema kuwa aliingia katika kikao cha Bodi ya Korosho kilichoandaliwa kutatua changamoto ya bei ya zao hilo na kukuta wahusika wa Bodi bila huruma wamependekeza kununua korosho kilo moja kwa shilingi 1500.

Rais Magufuli amesema kuwa hatuwezi kuendelea na hali hii yaani Mkulima ahangaike kulima kuweka mbolea kupulizia madawa kupalilia alafu kuja kulipwa kilo moja ya korosho shilingi 1500, hapo moja kwa moja unajua Bodi hii si kwa ajili ya wakiulima wa korosho.

Sasa mimi nikawapa bei elekezi iwe zaidi ya shilingi 3000 tukakubaliana lakini baadaye kwenye mnada wakafanya biashara wakapanga kuongeza shilingi moja, mbili, na bei ya juu zaidi wakaongeza  shilingi 16. Walifanya hivyo makusudio ili kuchelewesha ununuzi   mvua zianze kunyesha na katika kuokoa uharibifu wa korosho wakulima watashusha bei na wao wanunue kwa bei wanayoitaka.

Hata hivyo, kutokana na kukiuka makubaliano tuliyokubaliana sikuona tamko lolote  kuwakemea wafanyabiashara, wanunuzi wa korosho kutoka kwa Mawaziri wenye dhamana ambao ni Kilimo na Ushirika Viwanda na Biashara kwa nini wamekaaa kimya tu. Aliuliza Rais Magufuli.

Akielezea agizo lake kwa Wizara ya viwanda na Biashara kurejesha viwanda vilivoshindwa kufanya kazi amesema “Kiwanda cha Buco kilichopo Mkoa wa Lindi kilichorejeshwa serikalini na Wiaara ya fedha  na kiwanda cha Mponda kimerejeshwa na Waziri Mkuu na sio wizara husika kwa nini kazi zenu zifanywe na watu wengine. Sasa Mawaziri mnafanya kazi gani? 

Akijibu taarifa iliyowasilishwa na Waziri Mkuu Rais amesema kuwa sasa nimeamua  yafatayo: walioleta mapendekezo  ya kununua korosho achana  nao  watakuja  kutuchezea  tu, korosho tunanunua wenyewe. Korosho iliyobanguliwa kwa soko la ndani ndani ni kati ya shilingi 15,000 hadi 25,000 na tuna jumla ya tani laki mbili na elfu kumi hadi na Ishirini ukibangua korosho kilo tatu unapata kilo moja ya korosho iliyobanguliwa

Hivyo korosho zilizopo ni tani 210,000 mpaka 220,000 tukiibangua Watanzania milioni 35 kila mmoja atakula kilo mbili kwa bei nzuri tu alisisitiza Rais Magufuli akionyesha jinsi suala la Korosho lilivyorahisi na kwamba linakuzwa na wafanyabiashara wachache tu wenye nia ovu.
MALENGO   YA NCHI

Sisi tulipoomba ridhaa ya wananchi tulikuwa na malengo ni lazima tutatue masuala yote tuliyoahidi  ambayo tuliyaahidi mbele ya Bunge na yapo katika ilani ya chama chetu ni pamoja na changamoto ya masuala ya wakulima na wakulima ni asilimioia 70 ya Watanzania, hatuwezi  kuwafanya wakulima kuwa  vibarua wa watu wenye uwezo, alisisitiza Rais Magufuli.

Hasa katika sekta ya kilimo na viwanda ni sekta nyeti kwa Watanzania mara nyingi nimekuwa nikimuuliza Waziri Mkuu mbona hizi sekta haziendi vizuri panapotokea tatizo lazima yeye ashughulike . Mfano mwingine ni wakati wa tatizo la mbolea Kusini ilibidi Waziri Mkuu aende akamsimamie waziri na kazi ikafanyika, nikambwambia wakumbushe mawaziri wako ni lazima tuwe watumwa wa wananchi kwa kuwa tumejitoa kwa ajili ya watu.

Unappoona mahali pengine inabidi umtume waziri unajiuliza kuna nini tatizo la kawaha pale Kagera watu wanavusha kwa magendo kwenda nchi jirani ina maana Waziri wa viwanda ameshindwa kutafuta masoko kwa watu wake mpaka wanavusha kwa magendo nimemtuma waziri Mkuu ameenda kutatua.
‘’Tatizo la kiwanda cha Chai cha Mponde pale Bumbuli Lushoto kimekaa zaidi ya miaka mitatu bila kufanya kazi nimemtuma waziri Mkuu amekwenda ametatua  sasa unajiuliza waziri anafanya nini mwishowe nikamwambia sasa nitakufanya waziri wa Kilimo na Waziri wa Viwanda maana wewe unaweza kuondoa kasoro sasa hawa niliowaweka wanafanya nini’’?. alijiuliza Rais Magufuli
Rais Magufuli Akionyesha uwepo wa masoko nchi jirani mfano serikali ya Malawi imetenga Dola milioni 27.2 kwa ajili ya kununua mahindi, sasa kwa ni nni Wizara husika ya Viwanda Biashara na Masoko wasipate taarifa na kuzifanyia kazi wakulima wetu wapate soko la mahindi la uhakika badala yake wanahangaika kutafuta soko.

Aidha Rais alizipongeza wizara zinazofanya vizuri kama Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa chini ya Waziri Suleiman Jaffo ambaye ameweza kujenga vituo vya afya zaidi ya 300 na zahanati zaidi ya 60.

Pia, Rais  Magufuli amewashukuru Mawaziri waliopita Dkt Charles Tizeba na Charles Mwijage  kwa  kuwa  na moyo wa uzalendo na kushiriki katika kuapishwa Mawaziri  wapya wawili na Manaibu Waziri wanne. Hakika mmeonyesha moyo wa uzalendo na kuwaambia hizi kazi ni zetu wote unapoona umeshindwa kubali na kuwaachia wengine waaendelee.

Alitoa Taarifa kwa Rais Magufuli Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Majaliwa Kassim  amesema tani  90, 232  za korosho tayari zipo kwenye maghala makuu yanayosimamiwa na vyama vya ushirika. Pia bado kuna korosho ambazo ziko kwenye maghala ya AMCOS za wananchi ambazo zinasubiri kuondoa zilizopo katika maghala ya ushirika ili ziletwe.

Aidha, akieleza sababu za kushuka uzalishaji Waziri Mkuu Majaliwa amesema, “ :Mabadiliko ya hali ya hewa mwezi Septemba ambapo, kulikuwa na mvua na upepo mkali kwa hiyo uzal;ishaji kidogo utapungua kulinganishwa na mwaka jana ambazo zilikuwa tani laki 300 kwa mwaka huu uzalishaji unategemewa kuwa tani laki 220
AGIZO
Nawaagiza Jeshi la Wanznchi wa Tanzania-JWTZ kuanza operesheni Korosho mara moja mara nitoapo tamko . Mpaka sasa Wanajeshi wetu wapo Mkoa wa Lindi Mtwana na Ruvuma kwa ajili ya kazi ya kukusanya  korosho.

Aidha kiwanda cha BUCO kilichorejeshwa serikalini nawapa JWTZ, kama watatumia Jeshi la Kujenga Taifa –JKT katika kutoa nguvu kazi ya kubangua korosho nina hakika  kwao ni kazi rahisi kabisa. Pia, ghala lililopo  kiwandani hapo litumike kuhifadhi korosho itakayo kusanywa kutoka kwa wakulima.

Bodi zetu na Taasisi kama Tan trade, zifanye kazi ya kutafuta masoko Kituo cha Uwekezaji -TIC hakifanyi vizuri kutokana na kuingiliwa kiutendaji na Taasisi na Wizara nyingine sasa naagiza TIC ihamie Ofisi ya Waziri Mkuu, itakuwa rahisi kuratibu  vizuri zaidi na kwa ufanisi na wao kutoa maelekezo kwa Taasisi na Wizara husika. “Eyes on Hands Off”

Rais Magufuli amezitahadharisha Bodi zote kwa kusema kuwa kilichotokea Bodi ya  Korosho na Bodi ya Pamba ijiandae, pia mkazo utiliwe katika kutafuta masoko ya mazao ya Pareto, Kokoa , Ufuta na mazo mengine ili wakulima wanaolima kwa tabu wafaidike na matunda ya uwepo wa serikali yao.
Kwa wale Mawaziri mlioteuliwa msije mkajihusisha na kazi ya “Kang’omba” maana wako baadhi ya wafanyabiashara wanaofanya kazi ya Kang’omba ya kuweka Mawakala wao na jamaa zao ili kununua korosho tutajua mimi naombwa mkafanye kazi


Katika hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Manaibu Waziri walioapishwa ni Costantine Kanyasu kuwa Naibu waziri wa Maliasili na Utakii ,Dkt Mary Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora , awali alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika, Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara kuwa Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  na Mbunge wa Karagwe Mkoani Kagera Innocent Bashungwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika.


Hivyo makala

yaani makala yote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/na-judith-mhina-maelezo-rais-wa-jamhuri.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to " "

Post a Comment