title : KAMISHNA SURURU, AIPONGEZA UHAMIAJI KASKAZINI UNGUJA KUSOGEZA HUDUMA NDANI YA JAMII
kiungo : KAMISHNA SURURU, AIPONGEZA UHAMIAJI KASKAZINI UNGUJA KUSOGEZA HUDUMA NDANI YA JAMII
KAMISHNA SURURU, AIPONGEZA UHAMIAJI KASKAZINI UNGUJA KUSOGEZA HUDUMA NDANI YA JAMII
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (kati kati), akiwatoa hofu Watendaji wa Mamalaka ya Vitambulisho vya TAifa (NIDA) kwamba kuanzia mwezi January 2018, Idara ya Uhamiaji Zanzbar imejipanga kushughulikia maombi ya Vitambulisho vya Taifa kwa Raia wote watakaofika katika Ofisi yao iliyopo Kinduni, Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja, badala ya kufuata huduma Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini iliyopo Kivunge. Hatua hiyo ni utekelezaji wa Ahadi za Serikali kufikisha huduma karibu na Wananchi. Aliyasema hayo wakati alipotembelea Ofisi hizo wakati wa ziara ya kikazi katika Wilayani humo tarehe 05 - 06 Disemba, 2017.
Kamishna wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, amewapongeza watendaji wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa kusogeza huduma za Uhamiaji karibu na Jamii inayowazunguka. Alitoa pongezi hizo leo alipotembelea Vituo Maalum “Detached Points” vilivyopo ndani ya maeneo ya Kendwa na Nungwi, Shehia za Nungwi - Banda Kuu, Mnarani na Kiungani, Wilaya ya Kaskazini “A” na Fukwe za Kiwengwa, Pongwe na Pwani mchangani, Shehia za Kiwengwa, Moga na Pongwe kwa Wilaya ya Kaskazini “B” alipofanya ziara ya kikazi katika Wilayani hizo tarehe 05 – 06 Disemba, 2017.
Mkoa wa Kaskazini Unguja ni kitovu cha shughuli za Biashara na Uwekezaji katika sekta ya Utalii, hali inayosababisha kuwavuta wageni wengi kutoka Mataifa mbali mbali Duniani kutembelea maeneo hayo kwa madhumuni tofauti. “katika Mkoa huu Idara yetu ina kazi kubwa ya kuhudumia wageni wanaoingia na kuishi ndani ya Mkoa huu, kwani ni Mkoa ambao huwavuta wageni wanaokuja kutembea na kupumzika kwenye fukwe nadhifu, kuna wanaokuja kwa kuwekeza na wale wanaokuja kufanyakazi na biashara mbali mbali za Utalii, hali ambayo huibua changamoto nyingi za Kiuhamiaji” alisema Kamishna Sururu.
Kutokana na muingiliano huo wa wageni wa makundi tofauti, Idara ya Uhamiaji yenye dhamana ya kuhakikisha wageni wote wanaoingia na kuishi nchini wanafanya hivyo kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Uhamiaji, ina mchango mkubwa katika kuimarisha Ulinzi, Uchumi na Utamaduni wa watu wa Zanzibar. Kuanzishwa kwa Vituo maalum kwenye maeneo hayo ni mapinduzi makubwa katika Udhibiti na Usimamizi wa wageni wanaoingia na kuishi Zanzibar kinyume cha Sheria.
“Kwa kweli Nimefarijika sana kuona jinsi mlivyojipanga kuweza kuyafikia maeneo yote yenye changamoto za uwepo wa baadhi ya wageni wanaojipenyeza na kuishi nchini bila ya Kufuata Sheria za Uhamiaji. Uwepo wa Vituo hivi naamini ni muarobaini wa kuondoa kabisa tatizo la Uhamiaji haramu” Alisema Kamishna Sururu na kuongeza “Hatuzuwii wageni kuja kutembea, hatuzuwii wageni kufanyakazi ama kuwekeza nchini kwetu bali tunataka wageni wote waingie na kuishi nchini kwa kuheshimu Sheria za Nchi yetu, kwa kufanya hivyo tutaweza kufikia ile adhma njema ya serikali kufungua milango ya Biashara na Uwekezaji katika sekta ya Utalii kwa manufaa makubwa bila ya kuathiri Jamii na Tamaduni zetu”.
Hivyo makala KAMISHNA SURURU, AIPONGEZA UHAMIAJI KASKAZINI UNGUJA KUSOGEZA HUDUMA NDANI YA JAMII
yaani makala yote KAMISHNA SURURU, AIPONGEZA UHAMIAJI KASKAZINI UNGUJA KUSOGEZA HUDUMA NDANI YA JAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMISHNA SURURU, AIPONGEZA UHAMIAJI KASKAZINI UNGUJA KUSOGEZA HUDUMA NDANI YA JAMII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/12/kamishna-sururu-aipongeza-uhamiaji.html
0 Response to "KAMISHNA SURURU, AIPONGEZA UHAMIAJI KASKAZINI UNGUJA KUSOGEZA HUDUMA NDANI YA JAMII"
Post a Comment