title : MSHAMBULIAJI SIMBA AMFATA SAMATTA UBELGIJI
kiungo : MSHAMBULIAJI SIMBA AMFATA SAMATTA UBELGIJI
MSHAMBULIAJI SIMBA AMFATA SAMATTA UBELGIJI
Mshambuliaji wa Simba, Adam Salamba, yupo mbioni kutimkia kwenye Klabu ya Royal Sporting Club Anderlecht inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Mshambuliaji huyo mwenye mabao mawili katika ligi ya msimu huu, aliyejiunga Simba akitokea Lipuli msimu huu, amepata nafasi hiyo kutoka kwa wakala wa beki wa Rayon Sport, Abdul Rwatubyaye anayeishi nchini humo.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba, zinasema mchezaji huyo anatarajia kuondoka nchini Desemba, mwaka huu kwa ajili ya kufanya majaribio ya wiki moja kwenye timu hiyo inayokamata nafasi ya nne, mbele ya vinara wa ligi hiyo, KRC Genk anayoichezea Mbwana Samatta.
“Salamba anaweza kuondoka mwezi ujao kuelekea Ubelgiji kwenda Anderlecht kwa ajili ya kufanya majaribio ya wiki moja, kuna wakala wa huko ndiyo anafanya hiyo mipango ya kumpeleka baada ya kuvutiwa na uwezo wake kwani ameanza kumfuatilia tangu akiwa na Lipuli.
“Mipango ndiyo ipo kwenye mchakato wa kuweza kuona mambo yanakwenda vipi ila huyo wakala ndiye anajua kila jambo na mambo ya safari ingawa inafahamika kama atakaa huko kwa wiki moja katika majaribio yake,” alisema mtoa taarifa.
Championi Jumatatu lilimtafuta Mwenyekiti wa Simba, Swedy Mkwabi, akasema: “Bado sijapata taarifa za mchezaji huyo, hayo masuala ya timu yote yanajadiliwa kwanza na C.E.O ambaye ni (Crescentius) Magori pamoja na kocha kabla ya baadaye bodi kukutana na kujadiliana.”
Magori alipotafutwa jana, simu yake ya mkononi haikupokelewa
Hivyo makala MSHAMBULIAJI SIMBA AMFATA SAMATTA UBELGIJI
yaani makala yote MSHAMBULIAJI SIMBA AMFATA SAMATTA UBELGIJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MSHAMBULIAJI SIMBA AMFATA SAMATTA UBELGIJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mshambuliaji-simba-amfata-samatta.html
0 Response to "MSHAMBULIAJI SIMBA AMFATA SAMATTA UBELGIJI"
Post a Comment