title : BENKI ZINAZOTOA MIKOPO YA KILIMO TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZATAKIWA KUFUATA VIGEZO VYA UKOPESHAJI
kiungo : BENKI ZINAZOTOA MIKOPO YA KILIMO TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZATAKIWA KUFUATA VIGEZO VYA UKOPESHAJI
BENKI ZINAZOTOA MIKOPO YA KILIMO TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZATAKIWA KUFUATA VIGEZO VYA UKOPESHAJI
Na. WFM
Serikali imezitaka Benki zote zinazotoa mikopo ya kilimo
Tanzania Bara na Zanzibar kuhakikisha zinatoa mikopo kwa
kuzingatia vigezo vya ukopeshaji vikiwemo kuangalia
historia ya mkopaji ili kuondoa mikopo Chechefu (NPL).
Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa
akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Bububu Mhe.
Mwantakaje Haji Juma, aliyetaka kujua utaratibu
unaotumika kutoa mikopo kwa wakulima wa Zanzibar
kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).
Dkt. Kijaji alieleza kuwa kabla ya kutoa mkopo ni lazima
Benki ijiridhishe na aina ya mradi wa mkopaji ikiwa utaleta
faida itakayomuwezesha mkopaji kurejesha mkopo huo kwa
wakati ili kuzuia ukuaji wa Mikopo Chechefu.
Akijibu swali la msingi la Mbunge huyo aliyetaka kujua ni
wananchi wangapi wanaonufaika na mikopo ya Kilimo kwa
upande wa Zanzibar, Dkt. Kijaji alisema kuwa jumla ya
wananchi 3,000 wamenufaika na mikopo ya Benki ya TADB
hadi kufikia Julai 31, 2018.
“Kati ya wanufaika hao 3000, idadi ya wanaume
walionufaika ni 1800, wanawake 900 na vijana wa kike na
kiume ni 300”, alieleza Dkt. Kijaji.
Alisema kuwa jumla ya mikopo ya shillingi bilioni 6.50,
imetolewa kwa wananchi hao wa Zanzibar hadi kufikia Julai
31, 2018.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.
Hivyo makala BENKI ZINAZOTOA MIKOPO YA KILIMO TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZATAKIWA KUFUATA VIGEZO VYA UKOPESHAJI
yaani makala yote BENKI ZINAZOTOA MIKOPO YA KILIMO TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZATAKIWA KUFUATA VIGEZO VYA UKOPESHAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI ZINAZOTOA MIKOPO YA KILIMO TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZATAKIWA KUFUATA VIGEZO VYA UKOPESHAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/benki-zinazotoa-mikopo-ya-kilimo_11.html
0 Response to "BENKI ZINAZOTOA MIKOPO YA KILIMO TANZANIA BARA NA ZANZIBAR ZATAKIWA KUFUATA VIGEZO VYA UKOPESHAJI"
Post a Comment