title : Mabinti watakiwa kutumia tehama kuondoa changamoto katika jamii
kiungo : Mabinti watakiwa kutumia tehama kuondoa changamoto katika jamii
Mabinti watakiwa kutumia tehama kuondoa changamoto katika jamii
Na mwandishi wetu
KAIMU Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson amewataka mabinti wa Tanzania kufikiria taifa lao na namna ambavyo wanaweza kusaidia kuondoa changamoto mbalimbali zinazokabili jamii yao.
Kauli hiyo ameitoa katika jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali lililoshirikisha mabinti wa sekondari wa mkoa wa Dar es salaam; pamoja na mambo mengine walishiriki katika shindano la ubunifu wa programu za kompyuta.
Jukwaa hilo linalojulikana kama Girls Entrepreneurship Summit (GES) 2018 linachagiza mabinti kutumia Tehama kutatua matatizo yaliyopo katika jamii.
Jukwaa hilo lililoandaliwa na ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani nchini limelenga kusaidia mabinti kuchangia utatuzi wa matatizo kwa kuwa wabunifu katika ujasiriamali.
Kaimu Balozi huyo aliwataka mabinti hao kuwa na uvumilivu katika kukabiliana na changamoto zilizopo na kujenga mtandao ambao utawasaidia kuendelea mbele zaidi kiuchumi.
Alisema mtaji mkubwa wa wajasiriamali ni ubunifu na wazo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi bila kuogopa changamoto zilizopo.
Mapema katika hotuba yake Mwanzilishi mwenza wa Apps &Girls, Carolyne Ekyarisiima alisema kwamba jukwaa hilo na mashindano hayo yamelenga kuhakikisha kwamba binti anawezeshwa katika ulimwengu wa kidijiti kwa kumsogezea vishawishi mbalimbali vinavyompa motisha kuwa mbunifu kwa kutumia tehama.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson akizungumza na mabinti wa shule za sekondari za mkoa wa Dar es Salaam wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Afisa anayeshughulikia Utamaduni kutoka Ubalozi wa Marekani, Bw. Jeffrey Ladenson akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson (hayupo pichani) kufungua jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Mwanzilishi mwenza wa Apps & Girls, Bi. Carolyne Ekyarisiima akizungumzia shindano la ubunifu wa programu za kompyuta ambalo limelenga kuhakikisha kwamba binti anawezeshwa katika ulimwengu wa kidijiti wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Nancy Kaizilege akifafanua jinsi gani vijana wanavyoweza kubuni miradi inayolenga kufikia malengo ya maendeleo endelevu wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa
aadhi ya wasichana 156 kutoka shule 25 za Dar es salaam walioshiriki jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Dk. Inmi Patterson katika picha ya pamoja na wasichana 156 kutoka shule 25 za Dar es salaam wakati wa jukwaa la kufunza wasichana wajasiriamali (Girls Entrepreneurship Summit -GES 2018) lililoandaliwa shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Apps and Girls’ kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani na kufanyika katika ukumbi wa American Corner uliopo Maktaba Kuu ya Taifa.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Mabinti watakiwa kutumia tehama kuondoa changamoto katika jamii
yaani makala yote Mabinti watakiwa kutumia tehama kuondoa changamoto katika jamii Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mabinti watakiwa kutumia tehama kuondoa changamoto katika jamii mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mabinti-watakiwa-kutumia-tehama-kuondoa.html
0 Response to "Mabinti watakiwa kutumia tehama kuondoa changamoto katika jamii"
Post a Comment