title : VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI
kiungo : VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI
VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI
Vijana nchini watakiwa kubadili mtazamo kwa kuanzisha miradi ya kimkakati itakayowawezesha kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) alipofanya ziara hiyo Mkoa wa Iringa kwa lengo la Kuhamasisha na kukagua maeneo ya ujenzi wa Vitalu Nyumba (Green House) na uwepo wa miundombinu itakayotumika kwenye maeneo hayo.
Mheshimiwa Mhagama amesema sekta ya kilimo inaajiri na kuchangia katika pato la taifa kwa zaidi ya asilimia 60%, hivyo vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa wakatumie rasilimali ardhi kama mtaji wa kujiajiri na kuweza kuajiri wenzao.
“Lengo letu ni vijana kutumia sekta hii ya umahiri kwa ajili ya kuwaondoa kwenye mitazamo finyu na kuwa na mitazamo chanya ili waweze kunufaika na miradi itakayo buniwa na kutumika kama mfano kwa vijana nchi nzima.” Alisema Waziri Mhagama
Aliongeza kuwa vijana watafundishwa kilimo cha Kitalu nyumba ambavyo vitawawezesha kuongeza thamani kwenye mazao watakayozalisha na mradi huo ukawe sehemu ya ajira zao.Aidha, Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kuwa chachu ya maendeleo ya uchumi wa taifa kwa kushirikiana kwa pamoja bila kujali itikadi zao ili kutimiza adhima ya vijana wote.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Iringa mara baada ya kuwasili ofisini hapo kwa ajili ya ziara ya kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yaliyotengwa kujenga vitalu nyumba mkoani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akieleza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara mkoani humo ya kukagua maeneo ya kujenga vitalu nyumba. (Wa kwanza kushoto) ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bw. Fikira Kisimba.
Baadhi ya Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu waliombatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama katika ziara ya kukagua maeneo ya kujenga vitalu nyumba. (Kulia ni) Afisa Vijana Mwandamizi Bw. Gedfrey Massawe na Afisa Kazi Bi. Neema Moshi. (Kushoto ni) Afisa Elimu wa Mkoa Bw. Richard Mfugale.
Hivyo makala VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI
yaani makala yote VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/vijana-nchini-waaswa-kuanzisha-miradi.html
0 Response to "VIJANA NCHINI WAASWA KUANZISHA MIRADI YA KIMKAKATI"
Post a Comment