title : DC MJEMA ATOA SOMO KWA WAZAZI ,WALEZI KUPOROMOKA KWA MAADILI,AZITAKA SHULE BINAFSI KUSHIRIKIANA NA ZA SERIKALI.
kiungo : DC MJEMA ATOA SOMO KWA WAZAZI ,WALEZI KUPOROMOKA KWA MAADILI,AZITAKA SHULE BINAFSI KUSHIRIKIANA NA ZA SERIKALI.
DC MJEMA ATOA SOMO KWA WAZAZI ,WALEZI KUPOROMOKA KWA MAADILI,AZITAKA SHULE BINAFSI KUSHIRIKIANA NA ZA SERIKALI.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia (Nakivona ) Mjema akiwatunuku vyeti wahitimu wa Darasa la saba katika mahafali ya 24 ya shule ya msingi TUSIIME ambapo jumla yawanafunzi 245 wamehimu elimu ya Msingi.( Picha na Mwamba wa habari)
Mmoja wa wazazi waliofika katika sherhe za mahali ya darasa la saba shuke ya msingi TUSIIME akimtunza DC Mjema baada ya kuguswa na hotuba yake kuhusu malezi ya watoto na kushindwa kujizuia na kujikuta akitoa pochi na kutuza , DC mjema alitoa hotuba ambayo iligusa wazazi na wanafunzi.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema akimpa zawadimoja wa wanafuzi waliofanya vizuri katika mitihani.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Sophia Mjema akishukuru baada ya kupewa zawadi zawadi katika shule ya TUSIIME.
Mwamba wa habari.
Wazazi na walezi wametakiwa kuwa karibu na kufuatilia malezi ya watoto wao ilikuwajengea watoto msingi mzuri kimaisha moyo wa upendo jambo ambalo litawasaidia hata katika masomoyao waweze kufanya vizuri , kuwa wazalendo na raia wema katika Taifa.
Wito huo umetolewa na mkuu wa Wilaya ya Ilala alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya darasa la saba katika shule ya tusiime , na kuongeza kuwa watoto wengi wamengi wamekuwa na tabia mbaya kwa kukosa malezi ya familia na kuiga mambo ya kimagharibi na kuaziacha tamaduni za kitanzania jambo ambalo limechangia kuporomoka kwa maadili.
‘’Upendo wa familia unajengwa kwa familia kujumuika pamoja katika chakula cha jioni , Baba , Mama na Watoto na sikuiga mabo ya nje huko unakuta Wazi wako bize na mitandao ya kijamii na unakuta mwingine anawekewa chakula chumbani hayo siyo malezi, upendo nipale mnapokula katika mzunguko wa pamoja huyu anasema niongezee kawali ,Mamaniwekee juisi ,nibora wazazi tukatenga huo muda "alisema.
Aidha DC mjema amekemea vikali tabia za kuiga kutoka nchi zanje kila jambo kwa kuwa kuna mambo mengine yanayoigwa hana staha na heshima kwa jamii za kitanzania kwani mambo hayo yanachangia uharifu na uvunjifu wa maadili.
‘’ Kuna hiki kitu kina itwa sleep over sijui summer paty,vitu gani hivi vya kuiga vinatuharibia maadili ya watoto unakuta wanaalikana njoo na nightdress mzazi unajua wanaenda kufanya nini huko? Dont do that ,nasema hakuna sleep over hakuna kwa ninyi waswahili ni marufuku’’alionya DC Mjema .
DC Mjema pia amewataka wazazi kuwa waangalifu na watoto wao waliomaliza darasa la saba kwa kipindi hiki wakati wanangoja mhula wa kujiunga na kidato cha kwanza ili wasije kujiingiza katika makundi mabaya na kuangukia katika mikondo ya watu waharifu wakazimandotozao za kuendelea na masomo.
” Wazazi watoto hawa msiwaacha wakaanza kuzurula kuna simba huko watawararula usikubali kumwancha mtoto zaidi ya dakika tano bila kufahamu yuko wapi na anafanya nini , na ninyi watoto mtulie muache kuzurula hovyo “ alisema .
Pamoja na hayo DC Mjema amesema serikali ya awamu ya tano katika kuboresha elimu na kutoa fursa kwa kilamtoto wa Tanzania kupata elimu , imeamnua kutoa elimu bure na inaendelea kuboresha maslahai ya walimu ili kuinua kiwango cha elimu na amewataka wamiliki wa shule binafsi wilayani Ilala kushirikiana na shule za serikali kitaaluma na katika michezo kwani pamoja na kwamba shule zao ni za kulipia lakini wate wanajenga Taifa moja.
‘’Ninyi Tusiime mnao uwezo shirikianeni shule zetu za serikali mnzo maabara nzuri wakaribisheni wanafunzi na walimu wetu kujifunza hapa kwenu, pia natoa wito kwa shule zote zilizopo wilaya ya Ilala kuzingatia ratiba za michezo kwa watoto ilikuimarisha afya na kuvumbua vipaji vyao naninyi tusiime mpo mkiona shule zetu zinazubaa shulezetu zinajikongoja ingieni na waambieni mtafanya mashindano na kutoa mipira na viwanja nnaweza.''alisema
Kwa upande wake Mwalimu kuu wa shule ya Tusiime Philibert Simon , amesema shule hiyo imetatoa bure saili wa kidato cha kwanza kwa wahimu wa darasa la saba walio hitimu katika shule hiyo.
Shule ya TUSIIME ilianzishwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na imepata mafanikio makubwa katika Nyanja mbalimbali hasa kitaaluma, ambapo kwa kipindi chote hicho imeendelea kufanya vizuri katika mitihani ya ndani, mitahani ya kata , mitihani ya Wilaya , Mkoa na Taifa ambapo mwaka jana katika matokeo ya kumaliza Elimu ya Msingi ilishika nafasi ya 20 katiya shule 16,545 na kushika nafasi yatatu kimkoa na nafasi ya kwanza kiwilaya (Ilala) na mwanafunzi bora pia alitoka TUSIIME na kwa upande wa wasichana kumi bora mmoja alitoka shulehiyo.
Hivyo makala DC MJEMA ATOA SOMO KWA WAZAZI ,WALEZI KUPOROMOKA KWA MAADILI,AZITAKA SHULE BINAFSI KUSHIRIKIANA NA ZA SERIKALI.
yaani makala yote DC MJEMA ATOA SOMO KWA WAZAZI ,WALEZI KUPOROMOKA KWA MAADILI,AZITAKA SHULE BINAFSI KUSHIRIKIANA NA ZA SERIKALI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MJEMA ATOA SOMO KWA WAZAZI ,WALEZI KUPOROMOKA KWA MAADILI,AZITAKA SHULE BINAFSI KUSHIRIKIANA NA ZA SERIKALI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/dc-mjema-atoa-somo-kwa-wazazi-walezi.html
0 Response to "DC MJEMA ATOA SOMO KWA WAZAZI ,WALEZI KUPOROMOKA KWA MAADILI,AZITAKA SHULE BINAFSI KUSHIRIKIANA NA ZA SERIKALI."
Post a Comment