VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI

VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI
kiungo : VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI

soma pia


VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI


Na.Alex Sonna,Dodoma

Kufuatia ongezeko  la magari yanayoendeshwa na madereva wa Serikali kupata ajali, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Tanzania limeibuka na  kutoa tamko la kufuatilia na kuhakikisha madereva wanaoendesha magari ya viongozi wa Serikali wanapata mafunzo ya kuwaendesha viongozi hao.

Akizungumzana na waandishi wa habari Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo,Hamadi Masauni wakati akitoa tamko la kwanza mara baada ya kuchaguliwa kwa baraza hilo  huku akiwa ameongoza na Makamu Mwenyekiti wa baraza,Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Elias Kwandikwa na wajumbe wengine wa Baraza hilo.

Mhe.Masauni amesema kuwa baraza lilopita lilifanya kazi nzuri ila baraza jipya lina malengo yake ya kupunguza ajali nchini hasa za viongozi wa Serikari kwa kuwafuatilia na kuhakikisha madereva wanaoendesha magari hayo wanapata mafunzo ya kuwaendesha viongozi hao.

Aidha amesema kuwa kwa sasa wanaishauri Serikali kutoa waraka maalum utakaosaidia kuwadhibiti viongozi ambao wanatoa maelekezo kwa madereva wakimbize magari kwa mwendokasi na malengo ya baraza hilo ni kuimarisha utendaji wa kamati za usalama za mikoa na kuweka mikakati ya pamoja ya utendaji na usimamiaji wa majukumu ya kamati hizo.

“Kudhibiti mwendokasi na kuovateki kunakofanywa na madereva wa magari kwa kuwakamata,kuwaweka mahabusu na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao hivyo kukosa sifa ya kuondesha magari hayo,”amesema Masauni
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza hilo, ambapo aliwataka madereva wa magari ya Serikali kufuata sheria za barabarani na atakaye vunja sheria hizo atakamatwa, atawekwa mahabusu, kuwapeleka mahakamani  pamoja na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao na hivyo na hivyo kukosa sifa za kuendesha magari hayo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, jana.
PIX 2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na waandishi wa habari na wajumbe wa Baraza hilo, ambapo aliwataka madereva wa magari ya Serikali kufuata sheria za barabarani na atakaye vunja sheria hizo atakamatwa, atawekwa mahabusu, kuwapeleka mahakamani  pamoja na kuwaondolea sifa za madaraja C na E kwenye leseni zao na hivyo na hivyo kukosa sifa za kuendesha magari hayo. Kushoto meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dodoma, jana.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.




Hivyo makala VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI

yaani makala yote VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/vibarua-vya-madereva-wa-serikalini.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VIBARUA VYA MADEREVA WA SERIKALINI HATARINI"

Post a Comment