USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA

USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA
kiungo : USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA

soma pia


USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ushirikiano mzuri baina ya taasisi mbalimbali za dini nchini na Serikali ni jambo la muhimu katika kuboresha na kuimarisha amani.

Ameyasema hayo Jumatatu, Oktoba 22, 2018 alipowasili jijini Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako leo anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.

Alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, Waziri Mkuu amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo wa Serikali na wa dini mbalimbali.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mkakati wa viongozi wa dini wa kuunda kamati za amani nchini ambapo walianzia kwenye ngazi ya mkoa na sasa wamefikia katika kata.

“Viongozi wa dini mnadhamana kubwa katika kulifanya  Taifa liendelee kudumisha amani, utulivu na mshikamano, hivyo ushirikiano wenu na   Serikali ni muhimu.”

Amesema viongozi wa Serikali wakati wote wamekuwa tayari kufanyakazi na viongozi pamoja na taasisi mbalimbali za dini, lengo ni kuimarisha amani na utulivu uliopo nchini.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza inawajibu wa kuhakikisha kwamba maeneo ya mkoa huu yanaendelea kuwa salama.

Pia, Waziri Mkuu amempongeza Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hassan Bin Mussa Kabeke kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.

“Nakupongeza kaimu sheikh wa mkoa kwa kuteuliwa na ninakutakia kila la heri katika kazi yako na kwamba dhamana yako kubwa ni kuwaunganisha waislamu na waumini wa dini zote.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Hasani Bin Mussa Kabeke wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza  Oktoba 22, 2018 akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali.   Sheikh huyo amechaguliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella  (katikati) wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza akiwa njiani kwenda mkoani Simiyu ambako kesho anatarajia kufungua maonesho ya wajasiriamali. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Hivyo makala USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA

yaani makala yote USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/ushirikiano-wa-taasisi-za-dini-na_23.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "USHIRIKIANO WA TAASISI ZA DINI NA SERIKALI NI MUHIMU-MAJALIWA"

Post a Comment