TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA..YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA

TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA..YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA..YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA..YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA
kiungo : TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA..YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA

soma pia


TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA..YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesisitiza juu ya umuhimu wamiliki wa ving'amuzi na visimbuzi vinavyorusha matangazo yake hapa nchini kuheshimu sheria na kuhakikisha wana leseni zinazowaruhusu kuonesha chaneli za ndani bure badala ya kuwatoza wananchi fedha yoyote.

Hali hiyo imebainishwa leo Oktoba 3,2018 mjini Shinyanga kwenye semina ya siku moja iliyoendeshwa na Mamlaka hiyo kwa viongozi mbalimbali wa serikali, mashirika ya umma na asasi za kiraia mkoani Shinyanga.

Semina hiyo ililenga kuwapa uelewa viongozi hao juu ya sababu za TCRA kufungia baadhi ya ving’amuzi kurusha chaneli za ndani baada ya kubaini vimekiuka masharti ya leseni zao ambapo hata hivyo lengo ni kumwokoa mtumiaji wa ving’amuzi na visimbuzi kutotozwa gharama kubwa.

Mtoa mada katika semina hiyo, Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Francis Mihayo alisema lengo la mamlaka hiyo ni zuri ambalo limezingatia sheria za mawasiliano nchini.Mihayo alisema maamuzi yaliyochukuliwa na TCRA kuagiza kuondolewa kwa chaneli za ndani kwenye baadhi ya ving’amuzi na visimbuzi vya makampuni ya DSTV, AZAM TV na Zuku TV ambavyo havikuwa na leseni ya kurusha chaneli za ndani umelenga kusimamia sheria zilizopo.

Alisema ving’amuzi vilivyozuiliwa vinapaswa kuheshimu sheria za nchi na kwamba vituo vilivyoshinda tenda ya kuonesha chaneli za ndani zipatazo nane ndizo zinazopaswa kuonesha chaneli hizo na si vituo vingine.Alifafanua kuwa baada ya kuhama kutoka kwenye analojia kuja digitali, serikali iliweka sheria na taratibu ambazo zinatakiwa kufuatwa ili jamii iendelee kunufaika na uhabarishwaji pasipo kurudishwa nyuma na gharama kubwa.

"Kuna kitu kinaitwa FTA (hii ni ya kurusha Maudhui Bila kulipia) na vipindi vya kutolipia ni Vipindi vya Kijamii ikiwemo taarifa ya Habari, vinapaswa kuwa Bure.Na kuna mfumo wa (Subscription by payment) pay TV yaani watumiaji wanapata vipindi vya TV kwa kulipia, na hivi vipindi ni vile ambavyo si vipindi vya kijamii.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akifungua semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwa viongozi mbalimbali wa serikali, mashirika ya umma na asasi za kiraia mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapa uelewa viongozi hao juu ya sababu za TCRA kufungia baadhi ya ving’amuzi kurusha chaneli za ndani baada ya kubaini vimekiuka masharti ya leseni zao.Picha zote na Suleiman Abeid -Malunde1 blog.

Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Francis Mihayo TCRA Makao Makuu jijini Dar es Salaam akitoa mada wakati wa semina ya siku moja iliyoendeshwa na Mamlaka hiyo kwa viongozi mbalimbali wa serikali, mashirika ya umma na asasi za kiraia mkoani Shinyanga kwa ajili ya kuwapa uelewa viongozi hao juu ya sababu za TCRA kufungia baadhi ya ving’amuzi kurusha chaneli za ndani baada ya kubaini vimekiuka masharti ya leseni zao.

Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack wakisikiliza mada ukumbini.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia mada ukumbini.



Hivyo makala TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA..YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA

yaani makala yote TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA..YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA..YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tcra-yakutana-na-viongozi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TCRA YAKUTANA NA VIONGOZI SHINYANGA..YAWATAKA WAMILIKI WA VING'AMUZI NA VISIMBUZI KUHESHIMU SHERIA"

Post a Comment