title : WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUPIGA VITA MFUMO DUME
kiungo : WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUPIGA VITA MFUMO DUME
WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUPIGA VITA MFUMO DUME
Profesa Marjorie Mbilinyi akizungumzia simulizi ya hadithi yake Jijini Dar es Salam katika viwanja vya ofisi ya TGNP mtandao jinsi alivyofanikiwa kupambana kupiga vita mfumo dume usimtawale katika kutimiza ndoto zake.
rofesa Ruth Meena kushoto akimsikiliza kwa makini profesa Marjorie Mbilinyi Jijini Dar es salaam wakati wa kusimulia hadithi ya harakati za mapambano ya kujikwamua kuondokana mfumo dume.
Profesa Ruth Meena akiwa anawasimulia hadithi Wanafunzi wa vyuo vikuu Mbali mbali na wageni waalikwa Jijini Dar es Salaam namna alivyokuwa mwanaharakati wa kukataa kudidimizwa katika kujikwamua Kama mwanamke katika kujiendeleza kimasomo huku akiwa na majukumu ya kuangalia familia,pamoja na kufanya kazi.
Na Agness Francis,blogu ya jamii.
KATIKA harakati za ukombozi wa mwanawake,wanawake wametakiwa kuwa kipaumbele katika kuondokana na mfumo dume uliotawala katika jami yetu.
Ambapo wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuukataa na kupiga vita ukatili wa kijinsia,utabaka pamoja na ubeberu uliokithiri hasa kwa zile familia ambazo bado zinadhana potofu ya kumdidimiza mwanamke katika kupata Elimu na uongozi.
Amesema hayo Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TGNP mtandao Profesa Marjorie Mbilinyi wakati wa kilinge cha simulizi za hadithi za maisha yake alivyopambana mpaka hapo alipofikia pamoja na misuko suko yote aliyopitia akipindi akiwa binti mdogo lakini alihakikisha anaepukana na janga la kukandamizwa Kama mwanamke.
Profesa mbili ambaye ni mwanaharakati wa mabadiliko ya ukombozi wa mwanamke kimapinduzi wakati wa simulizi amesema kuwa hakuna utofauti sana wa ubaguzi huo hapa nchini kwetu na ulaya.
"Isipokuwa wanawake wa nchi za nje wamepiga hatua katika kujikomboa kuondokana na utabaka,ubepari,hivyo na sisi tujifunze kutoka kwao" amesema Profesa Mbilinyi.
Aidha mwanaharakati profesa Ruth Meena wakati wa simulizi wa hadithi yake amesisitiza kuwa wanawake wapige vikali vita ya mfumo huo wa unyonywaji na amewataka kusimama imara kupigania maendeleo na kutimiza ndoto zao.
Hata hivyo mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mlimani Sliyvia Sostenes baada ya simulizi hiyo amesema kuwa watakuwa mabalozi wazuri katika kuwaelemisha wengine ambao wapo katika janga hilo ili kuleta ukombozi wa mwanamke kimapinduzi.
Hivyo makala WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUPIGA VITA MFUMO DUME
yaani makala yote WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUPIGA VITA MFUMO DUME Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUPIGA VITA MFUMO DUME mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/wanawake-nchini-wametakiwa-kupiga-vita.html
0 Response to "WANAWAKE NCHINI WAMETAKIWA KUPIGA VITA MFUMO DUME"
Post a Comment