TAXIFY BODA YAZINDULIWA RASMI TANZANIA .

TAXIFY BODA YAZINDULIWA RASMI TANZANIA . - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAXIFY BODA YAZINDULIWA RASMI TANZANIA ., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAXIFY BODA YAZINDULIWA RASMI TANZANIA .
kiungo : TAXIFY BODA YAZINDULIWA RASMI TANZANIA .

soma pia


TAXIFY BODA YAZINDULIWA RASMI TANZANIA .

 Mwambawahabari
Kampuni ya Taxify imezindua huduma ya Taxify Boda jijini Dar es salaam na huduma hii sasa inapatikana katika jiji la Dar es salaam na Mwanza.

Huduma  hii inawezesha watanzania kupata usafiri wa bodaboda kwa kutumia teknologia ya Taxify App inayopatikana katika simu ya kiganja kwa urahisi na bei nafuu.

Tanzania ni nchi ya tatu ambapo huduma hiii imezinduliwa.
Bw. Shivachi Muleji Meneja Mkuu Afrika Mashariki wa Taxify, alisema kuwa kampuni ilibuni huduma hii ya Taxify Boda kutokana na kuongezeko kwa uhitaji wa usafiri wa usalama na uhakika wa pikipiki.

"Tatizo la foleni Dar es salaam umechochea ukuaji wa uhitaji wa usafiri wa pikipiki katika jiji la Dar es salaam, na uhitaji wa usafiri wa usalama na uhakika ni mojawapo ya kipaumbele kwa wasafarishaji na huduma yetu inatoa suluhisho kwa changamoto hizi” alisema
Bw. Remmy Eseka, Meneja Mkuu Tanzania alisema kuwa  huduma ya Taxify Boda imejikita katika kuhakikisha usalama wa madereva na abiria, na madereva wote ambao wamejisajili na huduma yetu wameelimishwa kuhusiana na hili.

 “Teknologia yetu inatuwezesha kufuatilia tabia ya madereva na huwezesha abiria uwezo wa kutoa maoni kuhusu huduma za dereva na safari yake kila anapotumia huduma zetu”

Kampuni imeweka mwongozo mkamilifu wa kuhakikisha usalama wa abiria. Wateja na madereva watahitajika kuvaa kofia ngumu na jaketi ya reflecta na tabia ya wateja kukaa upande ni marufuku kwa wateja na kuruhusiwa tu, kwa mteja aliye na ulemavu.

Pia, kuhakikisha usalama zaidi kwa wateja na madereva, kampuni inafutiliwa ushirkiano na makmpuni mbalimbali inayotoa huduma ya kwanza baada ya ajali na makampuni ambayo yanaweza kutoa usaidizi kwa dereva au abiria wakati wa dharura au ajali.

Kampuni imewekeza pia na mafunzo ziada ya udereva na huduma ya kwanza na kutoa vyeti kwa wote waliojisajili na huduma. “Tunatamani kupunguza pengo la ufanisi wa madereva kwa kutoa mafundisho na vyeti vya ubora,” alisema Eseka.  Pia kampuni itashirikiana na Jeshi la Polisi  kwa kutelekeza miongozo ya usalama.

Aidha Bw. Eseka alielezea kuwa huduma yao itasaidia madereva bodaboda kujiendeleza kila moja na maendeleo ya kibinafsi kutokana na mfumo wao wa biashara.

 "Tunataka kusaidia madereva wa pikipiki kufanya biashara zao kwa njia ya kitaaluma zaidi kwa kutoa jukwaa la kufuatilia safari, mapato na hata kupanga mipango ya maendeleo ya kibinafsi kama kujiunga na SACCO. Kwa kuwa sasa hivi madereva boda boda wanajitahidi kuanzisha makundi rasmi, Taxify Boda itatoa elimu kwa vikundi na hatimaye elimu itawasadia kuleta maendeleo kama kununua pipipiki,” alisema.

Eseka alielezea kuwa utoaji wa huduma ya teknologia inayounganisha abiria na madereva boda boda ni njia moja kampuni inachangia kuboresha muundo wa uchumi wa usafirishaji usio rasmi.


Hivyo makala TAXIFY BODA YAZINDULIWA RASMI TANZANIA .

yaani makala yote TAXIFY BODA YAZINDULIWA RASMI TANZANIA . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAXIFY BODA YAZINDULIWA RASMI TANZANIA . mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/taxify-boda-yazinduliwa-rasmi-tanzania.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAXIFY BODA YAZINDULIWA RASMI TANZANIA ."

Post a Comment