title : TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI KUFUZU AFCON
kiungo : TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI KUFUZU AFCON
TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI KUFUZU AFCON
TANZANIA imefufua matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde kwenye mchezo wa Kundi L jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.Ushindi huo wa kwanza kwenye mashindano haya, unaifanya Taifa Stars ijisogeze hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo, ikifikisha pointi tano baada ya kucheza mechi nne, ikifungwa moja na sare mbili.
Uganda ambayo usiku huu inamenyana na Lesotho mjini Maseru, ndiyo inaongoza kundi hilo kwa pointi zake saba za mechi tatu, wakati Cape Verde inabaki na pointi zake nne katika nafasi ya tatu. Lesotho ndiyo inashika mkia kwa pointi zake mbili.
Hadi mapumziko, Taifa Stars walikuwa mbele kwa bao 1-0 lilillfungwa na kiungo mshambuliaji wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco, Simon Msuva dakika ya 29 akimalizia pasi nzuri ya Nahodha, Mbwana Samatta aliyemtoka beki wa kushoto wa Papa wa Bluu, Rodrigues Carlos.
Hivyo makala TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI KUFUZU AFCON
yaani makala yote TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI KUFUZU AFCON Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI KUFUZU AFCON mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/taifa-stars-yafufua-matumaini-kufuzu.html
0 Response to "TAIFA STARS YAFUFUA MATUMAINI KUFUZU AFCON"
Post a Comment