title : TAASISI YA ROOM TO READ YAPUNGUZA KASI ZA MIMBA ZA UTOTONI KUTOKA ASILIMIA 18 %HADI 1%
kiungo : TAASISI YA ROOM TO READ YAPUNGUZA KASI ZA MIMBA ZA UTOTONI KUTOKA ASILIMIA 18 %HADI 1%
TAASISI YA ROOM TO READ YAPUNGUZA KASI ZA MIMBA ZA UTOTONI KUTOKA ASILIMIA 18 %HADI 1%
IMEELEZWA kuwa Mkoa wa Pwani umefanikiwa kutokomeza mimba za utotoni na utoro mashuleni kwa watoto wa kike kutoka asilimia 18 hadi kushuka kiwango hicho na kufikia asilimia moja.
Yamesema hayo na Mkurugenzi Mkazi kutoka Taasisi ya Room to Read Peter Mwakabwele aliyezungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoka 11 kila mwaka.
Amesema kuwa taasisi hiyo ya Room to Read ilijikita katika Mkoa wa Pwani na kuweka mikakati ya kusimamia haki ya kupata elimu kwa watoro wa kike ambao wanaishi katika mazingira magumu na kuwapa msaada wa kuwapeleka shule na kuwasimamia katika ngazi ya shule za msingi, sekondari na hata wanao pata nafasi ya kuendelea katika ngazi za elimu ya juu.
"Room to Read tumeweza kufanikisha tunapunguza kasi ya ndoa za utotoni na utoro mashuleni kwa kwa watoto wa kike kwa kuhakikisha karibu na wazazi wa mabinti gao na kufuatilia maendeleo yao ya masomo na kuwaelewesha wazazi umuhimu wa mtoto wa kike kupata elimu" alisema Mkurugenzi huyo.
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa miaka mingi nyuma Mkoa wa Pwani ulikua ukiongoza kwa ndoa za utotoni na utoro shuleni jamabo ambalo lilichangiwa na mila na desturi za unyago wa kuwaweka ndani mabinti na kuwacheza ngoma wakati wenzao wakiendelea na masomo huku wengine wakiozeshwa baada ya kuchezwa lakini hivi sasa hali imebadilika kwani mabinti hao wamekuwa wakiongoza kwa ufaulu kwenye mitihani ya kitaifa.
Amekwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa Room to read wamekuwa wakitumia mbinu za hali ya juu kwa kuwaweka karibu na kuwasikiliza ikiwemo kuwafundisha stadi za maisha ili waweze kujiongoza kielimu na kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika maisha ya kila siku na hata familia kwa ujumla.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa Taasisi hiyo ya Room to Read imekuwa ikitoa bure sare zashule , kuwalipia ada za shule na bweni kwa wanaoishi mbali na shule, pia huwapatia chakula na usafiri wa kwenda na kurudi shuleni pia wapo ambao wamenunuliwa baiskeli ili kuwarahisishia kwenda shuleni pia wanao wasimamizi na wagamasishaji ambao huwa nao kwa muda wote ili kuhakikisha lengo la kumkomboa mtoto wa kike linatimia.
Amesema kuwa tayari mradi huo wa Room to Read umefanikiwa kuwasomesha wanafunzi wa kike zaidi ya 3500 ambao tayari wamesha hitimu katika viwango vya ngazi mbalimbali vya elimu huku wengine wakiwa nje ya nchi wakijiendeleza na masomo ya elimu ya juu.
Hivi sasa wanao wanafunzi wanaowasimamaia 8000 ambao wako katika shule ya msingu huku katika sgule za sekondari wako wanafunzi zaidi ya 2,900.
Aidha amezitaja Wilaya ambazo zinanufaika na mradi huo kuwa ni Kibaha, Bagamoyo na Chalinze pia amesema kuwa katika kipindi cha mwaka huu mradi huo umefanikiwa kutanuka baada ya kuongeza kipengele cha kuwawekea somo la biashara ili wale watakaofeli waweze kujiendeleza kibiashara na kujiajiri ili kuweza kujikimu kimaisha.
Naye Katibu tawala wa Mkoa wa Pwani Mama Theresia Mbwambo amesema kuwa amewapongeza wadau wa mradi huo wa Room to Read kwa kumkumbuka mtoto wa kike na kufanikiwa kumkomboa kielimu.
"Tunatarajia kwamba hivi sasa watoto wetu wa kike watafanikiwa kusoma vema kama jinsi walivyopanda katika ufaulu kwenye darasa la saba na mitihani ya kidato cha nne"alisema Mama mbwambo.
Naye Afisa habari wa Mkoa wa Pwani Alhaji Maulid Abdul amesema kuwa serikali ya awamu ya tano ni serikali makini na kamwe haitovumilia vitendo vya wazai kuwacheza ngoma watoto wakati wa kipindi cha masomo.
"Hatuzikatai mila na desturi ni nzuri lakini ku a baadhi ya mila inabidi tuziache"alisema
Mkurugenzi Mkazi kutoka Taasisi ya Room to Read Peter Mwakabwele akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani mkoani Pwani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoka 11 kila mwaka. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa mradi wa Room to Read Zamaradi na wa pili kulia ni Afisa elimu mkoa wa Pwani Alhaj Maulid Abdul nanaliyeketi mwenyw ushungi
Mrisho Mpoto pamoja na wasanii wengine wakitoa burudani katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoka 11 kila mwaka yaliyofanyika mkoani Pwani.
Hivyo makala TAASISI YA ROOM TO READ YAPUNGUZA KASI ZA MIMBA ZA UTOTONI KUTOKA ASILIMIA 18 %HADI 1%
yaani makala yote TAASISI YA ROOM TO READ YAPUNGUZA KASI ZA MIMBA ZA UTOTONI KUTOKA ASILIMIA 18 %HADI 1% Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAASISI YA ROOM TO READ YAPUNGUZA KASI ZA MIMBA ZA UTOTONI KUTOKA ASILIMIA 18 %HADI 1% mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/taasisi-ya-room-to-read-yapunguza-kasi.html
0 Response to "TAASISI YA ROOM TO READ YAPUNGUZA KASI ZA MIMBA ZA UTOTONI KUTOKA ASILIMIA 18 %HADI 1%"
Post a Comment