title : NAIBU MEYA ILALA AKUTANA NA UWAVI AWAAHIDI MAKUBWA.
kiungo : NAIBU MEYA ILALA AKUTANA NA UWAVI AWAAHIDI MAKUBWA.
NAIBU MEYA ILALA AKUTANA NA UWAVI AWAAHIDI MAKUBWA.
Naibu meya wa MKanispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto ,aliye katikati wengine ni wanachama wa UWAVI wakimsikiliza kwamakini alipokutana nao Vingunguti .
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , ambaye piaDiwani wa Kata ya vingunguti Omary Said Kumbilamoto leo amekutana na Umoja wa walemavu wa kata hiyo (UWAVI) kusikiliza kero zao na kujadili fursa za kiuchumi zitakazo wawezesha kujitegemea.
Akizungumza katika mkutano huo Kumbilamoto, amewataka walemavu hao kujitokeza kwa wingi kuchukua mikopo ya walemavu inayotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ili waweze kujiendeleza kibiashara kwa na kuacha utegemezi kwa kuwa wanao uwezo wa kufanya kazi.
“Fedha zenu zipo Halmashauri na nimezungumza katika Baraza la madiwani, ninyi mpewe kipaumbele,nimedhamiria kuwa saidia nataka niwaambie ninyi mna weza wala msijisikie wanyonyonge na Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inawajailisana na wasaidizi wake hatutawaacha pekeyenu na mimi nawaahidi ntawatafutia wadau na mtakapofungua Account CRDB watakuwa wanawaingizia pesa” alisema.
“Fedha zenu zipo Halmashauri na nimezungumza katika Baraza la madiwani, ninyi mpewe kipaumbele,nimedhamiria kuwa saidia nataka niwaambie ninyi mna weza wala msijisikie wanyonyonge na Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inawajailisana na wasaidizi wake hatutawaacha pekeyenu na mimi nawaahidi ntawatafutia wadau na mtakapofungua Account CRDB watakuwa wanawaingizia pesa” alisema.
Aidha Kumbilamoto ,amesema kutokana na changamoto zinazo wakabila walemavu hao, ameahidi kuwaletea Afisa maendeleo wa Manispaa ili aweze kuwapa elimu kuhusu mikopo na mbinu za kuibuafursa za kizakibiashara kwakuwa mpaka sasa hawaja pata biashara ya kufanya.
Hatahivyo walemavu hao wameeleza ugumu wa dhamana ya mikopo iliyowekwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ikwemo dhamana ya nyumba ambapo wamesema sharti hilo nigumu na kuomba mashart yalegezwe na kuondolewa kwa shart la nyumba kwa kuwa wengi wao wanaishi kwenye nyumba za kupanga.
Umoja wa walemavu Kata ya Vingunguti (UWAVI) unawanachama wapatao 70 ,ambao wote wanategema mikopo hiyo ili waanze kujishughu;lisha na biashara ndogondogo, na umoja huo uko katika hatua za mwisho za usajili .
Hivyo makala NAIBU MEYA ILALA AKUTANA NA UWAVI AWAAHIDI MAKUBWA.
yaani makala yote NAIBU MEYA ILALA AKUTANA NA UWAVI AWAAHIDI MAKUBWA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU MEYA ILALA AKUTANA NA UWAVI AWAAHIDI MAKUBWA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/naibu-meya-ilala-akutana-na-uwavi.html
0 Response to "NAIBU MEYA ILALA AKUTANA NA UWAVI AWAAHIDI MAKUBWA."
Post a Comment