title : SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL YAFANYA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE TANGU KUANZISHWA KWAKE
kiungo : SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL YAFANYA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE TANGU KUANZISHWA KWAKE
SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL YAFANYA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE TANGU KUANZISHWA KWAKE
SHULE ya sekondari ya Imperial kwa mara ya kwanza imesheherekea
mahafali ya kwanza ya kidato cha nne mahafari yaliyofanyika jana Oktoba 20,2019.
Akizungumza Katika mahafali hayo Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda alisema kuwa shule zinajukumu la kuwaandaa vijana kuwa Viongozi Bora kwani waliowengi hutokea shuleni.
Pia alizindua kampeni maalum ya Shule hiyo inayotambua mchango wa viongozi mbalimbali katika kuhamasisha uongozi bora, alisema wanafunzi wanaoaminishwa kuwa wanaweza kuwa viongozi bora tangu wakiwa wadogo hujenga tabia ya wao kujilinda na kujichunga wenyewe.
Mbali na kusifia mandhari nzuri ya shule hiyo Anne alisema anaamini Viongozi wazuri watatoka shuleni hapo, na kuwasihi wazazi kutohangaika kuwapeleka watoto wao mbali ili hali kuna shule kama Imperial yeye viwango vya kimataifa.
Kwa Mujibu wa Mkuu wa Shule hiyo bwana Lincolin Mashanda, alisema nayo Imperial Sec School imejiandaa kuzalisha Viongozi hao wa Kesho katika fani na nyanja mbalimbali katika ubora kwa kuzingatia, maadili mema na kwa kuhamasisha hilo kuanzia Shuleni hapo.
Mashanda amesema
"Yapo mambo kadhaa ambayo yanamfanya mtu awe kiongozi bora, mambo haya yakianza kuzoeshwa mapema huwa tabia na muongozo kwa vijana wetu..
Mashanda alikinukuu Kituo cha utafiti na mafunzo ya uongozi cha Dale Carnegie cha jijini New York nchini Marekani kinachosema katika utafiti wao wamegundua kwamba kinachomfanya mtu awe kiongozi bora sio suti wala sura bali uwezo na nia ya dhati katika kuamsha ari, kuwawezesha unaowaongoza, kuwafanya wajiamini na kuwapa motisha watu unaowaongoza.
Kiongozi bora ni yule anayeweze Kuyakabili Matatizo au Changamoto
Kiongozi bora ni yule ambaye ana ujasiri wa kutosha wa kukabiliana na kila aina ya changamoto inaweza kujitokeza kwa busara."
"Dunia ya leo imejaa changamoto za kila aina. Kila kukicha kuna jipya na gumu zaidi. Taswira ya uingozi bora inamjenga kijana kujiamini na kujilinda hivyo kuwa sababu ya yeye kukabiliana na changamoto mbalimbali za ujana kwa matumaini."
"Kiongozi bora lazima awe muaminifu. Uaminifu unaanzia kwenye kuwa mkweli. Na hii nitabia inayoanza utototoni."
"Kiongozi bora ni yule mwenye uwezo wa kusimamia ahadi yake na jitihada anazofanya kutimiza ahadi yake."
"Kiongozi bora lazima ajiheshimu. Na dhana ya kujiheshimu ni pana. Hii ni pamoja na kuheshimu wazazi wako, ndugu, jamaa marafiki na watu wote. Unapojiheshimu, inakuwa rahisi kuongoza wengine."
:Kiongozi bora huwa anakiu ya kujifunza zaidi na ni mtafiti.
Kiongozi bora ni Mtendaji
Yote niliyoyataja hapo yanafundishika."
:Sasa pamoja na masomo mengine Imperial secondary school inamuandaa mwanafunzi wake katika mazingira ya kuyatambua haya na kuyafanyia kazi mapema kipindi awapo shuleni. '
Alisema 'Tunaamini ugeni wa mama Anne S..Makinda katika mahali yetu utaongeza tija na hamasa kwa kile tulichokuwa tukiwaandaa nacho wanafunzi wetu.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne wakiwa katika picha ya pamoja.
Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne Imperial Secondary School (ISS) yaliyofanyika jana Msolwa Chalinze.
Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusheherekea Mahafari ya kwanza ya kidato cha nne.

Mgeni Rasmi ambaye ni Spika wa Bunge Mstaafu Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu pamoja na wazazi wao katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne.
Hivyo makala SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL YAFANYA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE TANGU KUANZISHWA KWAKE
yaani makala yote SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL YAFANYA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE TANGU KUANZISHWA KWAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL YAFANYA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE TANGU KUANZISHWA KWAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/shule-ya-sekondari-imperial-yafanya.html
0 Response to "SHULE YA SEKONDARI IMPERIAL YAFANYA MAHAFALI YA KIDATO CHA NNE TANGU KUANZISHWA KWAKE"
Post a Comment