title : SERIKALI HAITAMWONEA HURUMA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU-NAIBU WAZIRI ULEGA
kiungo : SERIKALI HAITAMWONEA HURUMA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU-NAIBU WAZIRI ULEGA
SERIKALI HAITAMWONEA HURUMA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU-NAIBU WAZIRI ULEGA
Serikali imepiga marufuku uvuvi haramu na kuteketeza nyavu aina ya makokoro 35 , makila 6 na nyavu za zenia 25 zilizokuwa zikitumiwa na wavuvi haramu katika bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kagongo kata Lang’ata leo,Naibu Waziri wa mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega amesema serikali haitamwonea huruma mtu yeyote atakayekamatwa akijihusisha na uvuvi haramu kwani serikali imekua ikipoteza kiasi kikubwa cha mapato kutokana na uvuvi huo.
“Hatuna utani na mtu asiye na huruma na rasilimali za nchi hii, Tanzania ndio nchi yenye sehemukubwa yenye maji kuliko sehemu nyingine lakini bado tunaagiza samaki kutoka nchini china, tumeagiza sato., perege hadi kibua wa kichina, tusipotokomeza leo bwawa litakuwa historia kwa vizazi vijavyo” amesema Ulega
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira alisema uwepo wa bwawa hilo umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika eneo hilo na sasa ni wakati wa wananchi kuwa walinzi kwa kila mmoja ili kutokomeza uvuvi haramu.“Hebu leo amueni kabisa kwamba biashara ya samaki ndio mfumo wa maisha yenu, Ninyi mkifanya hivyo sisi hatutahitaji kufunga hili bwawa , wakati wote tutahitaji kuongeza kizazi cha samaki na kuleta wataalamu kupima kiwango cha samaki tulichonacho” alisema Mghwira
Kwa upande wake Dismas Gondwe mkazi wa kijiji cha kigongo kata ya Lang’ata amesema uvuvi haramu katika bwawa hilo unatokana na kukosekana kwa utaratibu maalumu unaowaelekeza wavuvi kuendesha shughuli zao katika bwawa hilo.
Gondwe ameiomba serikali kuwawezesha wavuvi wa bwawa la Nyumba ya Mungu zana harali ambazo serikali inazitambua.
Naibi Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi wa kijiji cha Kagongo kata ya Lang`ata mkoa wa Kilimanjaro kuhusu serikali kutokumuonea huruma mtu yoyote ambaye atajihusisha na shughuli za uvuvi haramu.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG Kilimanjaro)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira.
Naibi Waziri Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wakwanza kulia) kwa kushirikiana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira na Mkuu wa wilaya ya Mwanga Aarron Mbogho wakiteketeza zana haramu zilizokua zikitumika katika uvuvi haramu kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG Kilimanjaro)
Sehemu ya wavuvi wa kijiji cha Kagongo kata ya Lang`ata mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega.
Zana haramu zilizokua zikitumika katika uvuvi haramu zikiteketezwa
Hivyo makala SERIKALI HAITAMWONEA HURUMA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU-NAIBU WAZIRI ULEGA
yaani makala yote SERIKALI HAITAMWONEA HURUMA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU-NAIBU WAZIRI ULEGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI HAITAMWONEA HURUMA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU-NAIBU WAZIRI ULEGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/serikali-haitamwonea-huruma-mtu-yeyote.html
0 Response to "SERIKALI HAITAMWONEA HURUMA MTU YEYOTE ATAKAYEKAMATWA AKIJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU-NAIBU WAZIRI ULEGA"
Post a Comment