title : PROF.KAMUZORA: JAMII INAPASWA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOWAKANDAMIZA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI
kiungo : PROF.KAMUZORA: JAMII INAPASWA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOWAKANDAMIZA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI
PROF.KAMUZORA: JAMII INAPASWA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOWAKANDAMIZA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI
NA MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu Prof.Faustin Kamuzora ameiasa jamii kutokomeza mila na desturi potofu zinazokwamisha maendeleo ya wanawake na watoto sambamba na kuwapatia fursa ya kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Wito huo ameutoa Oktoba 26, 2018 wakati akifungua mkutano wa Kamati Elekezi ya Taifa ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto uliohusisha Wizara 11 pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya wanawake na watoto nchini walipokutana mkoani Morogoro kujadili na kupitia Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.
“Jamii inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kupinga mila na desturi potofu zinazokandamiza makundi haya na badala yake kutumia muda mwingi katika kuzalisha mali na kujishughulisha katika masuala ya maendeleo ili kuondokana na umasikini na kujiletea maendeleo”.alisema Kamuzora
Aidha Kamuzora aliongezea kuwa, jamii inapaswa kuendelea kusaidia jitihada za Serikali katika kutokomeza mila na desturi potofu kwa kuunga mkono mipango mikakati iliyopo na kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya Haki na Usawa katika jamii.
“Tujitathimini na kuona namna bora ya kuondokana na mila na desturi zote zinazomkandamiza wanamke na mtoto ili kuendelea kusimamia zile zinazoiwezesha jamii kuwa na usawa na haki katika makundi yote bila kuwa na ubaguzi”
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof.Faustin Kamuzora (Kulia) akifungua kikao cha Kamati elekezi ya Taifa ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto kwa ajili ya kujadili Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kilichofanyika Mkoani Morogoro Oktoba 26, 2018 kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. John Jingu.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt.Laurean Ndumbaro akizungumza wakati wa kikao cha Kamati elekezi ya Taifa ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto kwa ajili ya kujadili Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kilichofanyika Mkoani Morogoro Oktoba 26, 2018 kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw.Amoni Mpanju.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya (Maendeleo ya jamii) Bw.Mwambene Atupele akichangia jambo wakati wa kiako hicho.
Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) kutoka Wizara ya Viwanda Bi.Zaytun Bagholleh akifafanua jambo wakati wa kikao kazi hicho.
Mjumbe kutoka UNICEF Bi.Maud Droogleever akichangia jambo kuhusu ushirikishwaji wa Taasisi zisizokuwa za Kiserikali katika mapambano dhidi ya Utatili wa wanawake na watoto wakati wa kikao kazi hicho.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala PROF.KAMUZORA: JAMII INAPASWA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOWAKANDAMIZA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI
yaani makala yote PROF.KAMUZORA: JAMII INAPASWA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOWAKANDAMIZA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROF.KAMUZORA: JAMII INAPASWA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOWAKANDAMIZA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/profkamuzora-jamii-inapaswa-kutokomeza.html
0 Response to "PROF.KAMUZORA: JAMII INAPASWA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI ZINAZOWAKANDAMIZA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI"
Post a Comment