TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA

TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA
kiungo : TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA

soma pia


TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inathamini uwepo wa sekta binafsi nchini na kwamba inaendelea kushirikiana nayo katika kuboresha maendeleo ya Taifa.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Oktoba 27, 2018) wakati alipokutana na bodi mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania kwenye makazi wa Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ampongeza Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw. Salum Shamte na wajumbe wa bodi hiyo kwa kuchaguliwa kuingoza taasisi hiyo. Bodi hiyo mpya ilikwenda kujitambulisha.

“Serikali inadhamira ya dhati ya kushirikiana na taasisi hii kwa sababu ndio muwezeshaji wa kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025,” amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa taasisi hiyo Bw. Shamte amesema sekta binafsi inatambua juhudi za Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara nchini Tanzania.

“Sisi tupo tayari kushirikiana na Serikali kwa kuwabana wafanyabiashara ambao wanaenda kinyume na maadili na sheria, ila tunaomba Serikali ishirikiane nasi katika utekelezaji wake.”

Pia, Bw. Shamte ameiomba Serikali iendelee kutoa vivutio kwa biashara zinazoanza ili kuhamasisha uwekezaji kwa kuwa baadhi yake zimeonesha gharama kubwa za uzalishaji.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Bodi Mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dsr es salaam Oktoba 27, 2018.  Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustin Kamuzora na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Salum Shamte. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi Mpya ya Taasisi  ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) baada ya mazungumzo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Oktoba 27, 2018. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustin  Kamuzora  na kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Salum Shamte.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Salum Shamte  baada ya kukutana na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Oktoba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Hivyo makala TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA

yaani makala yote TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tutaendelea-kushirikiana-na-sekta.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA"

Post a Comment