title : PROFESA LIPUMBA, SAKAYA KUWEKA KAMBI KULINDA NGOME YA CUF LIWALE , WAMCHAMBUA MGOMBEA WA CCM.
kiungo : PROFESA LIPUMBA, SAKAYA KUWEKA KAMBI KULINDA NGOME YA CUF LIWALE , WAMCHAMBUA MGOMBEA WA CCM.
PROFESA LIPUMBA, SAKAYA KUWEKA KAMBI KULINDA NGOME YA CUF LIWALE , WAMCHAMBUA MGOMBEA WA CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na Kaimu Katibu Mkuu Magdalena Sakaya anatarajia kwenda kufunga kampeni za uchaguzi mdogo katika Jimbo la Liwale ili hukakikisha chama hicho kinateta nafasi katika jimbo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa Profesa Lipumba, amesema kuwa anakwenda kuwaongoza wanachama wa CUF na wakazi liwale ili waipigie kura ya ndio kwa wagombe wa CUf katika nafasi ya Ubunge na udiwani.
"Utafiti wa siasa katika wilaya liwale unaonesha wazi CUF ina wanachama wengi, katika uchaguzi mwaka 20I5 Mgombea wa CUF alipata kura nyingi kuliko wagombea wote wa ACT, ADC, CCM na CHADEMA" amesema Profesa Lipumba.
Amesema kuwa Mgombea wa CCM katika Jimbo la Liwale Mhe. Mohamed Zuberi Kuchauka mwaka 20I5 alishinda Ubunge kutokana chama cha CUF kinakubalika Liwale na sio yeye binafsi anakubalika.
"Baada ya kupata Ubunge hakuweka mipango yoyote ya kutimia ahadi zake na alikuwa hayupo karibu na wananchi wake, ndani ya CUF alionekana mzigo" amesema Profesa Lipumba.
Profesa Lipumba amesema kuwa Mgombea wa CUF katika Jimbo la Liwale ni Mhe. Mohamed Rashid Mtesa ambaye ni diwani wa Kata ya Liwale B na Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale.
"Mhe. Mtesa nakubalika liwale kwa sababu ya kuongoza vizuri halmashauri ya liwale, ni mtu wa watu, hana makuu na hata watendaji wa serikali wanamheshimu na kukubalika kwa sababu ya uadilifu katika uongozi wake" amesema Profesa Lipumba.
Hata hivyo ameeleza kuwa msimamizi wa uchaguzi anatakiwa kuwaacha wananchi kumchagua kiongozi wanayemtaka kuliko kuwachagulia kiongozi wasiyemtaka.
"Tunaomba katika uchaguzi busara na hekima itumike, tunajua CCM wamefanya makosa kumteuwa Mohammed Kachauka kuwa mgombe wao, Liwale ni ngome ya CUF" amesema Profesa Lipumba.
Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Liwale umetokana na Mbunge wa Liwale kwa tiketi ya CUF Mohammed Zuberi Kachauka kujivua uanachama wa CUF na kujiunga na CCM.
Hivyo makala PROFESA LIPUMBA, SAKAYA KUWEKA KAMBI KULINDA NGOME YA CUF LIWALE , WAMCHAMBUA MGOMBEA WA CCM.
yaani makala yote PROFESA LIPUMBA, SAKAYA KUWEKA KAMBI KULINDA NGOME YA CUF LIWALE , WAMCHAMBUA MGOMBEA WA CCM. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROFESA LIPUMBA, SAKAYA KUWEKA KAMBI KULINDA NGOME YA CUF LIWALE , WAMCHAMBUA MGOMBEA WA CCM. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/profesa-lipumba-sakaya-kuweka-kambi.html
0 Response to "PROFESA LIPUMBA, SAKAYA KUWEKA KAMBI KULINDA NGOME YA CUF LIWALE , WAMCHAMBUA MGOMBEA WA CCM."
Post a Comment