title : Mhini aenda kujiunga St Felix Uingereza, aahaidi kuleta medali ya kwanza ya kuogelea Tanzania
kiungo : Mhini aenda kujiunga St Felix Uingereza, aahaidi kuleta medali ya kwanza ya kuogelea Tanzania
Mhini aenda kujiunga St Felix Uingereza, aahaidi kuleta medali ya kwanza ya kuogelea Tanzania
Muogeleaji, Dennis Mhini (wa nne kutoka kulia) akiwa na wazazi wake na ndugu na jamaa kabla ya kuondoka kwenda nchini Uingereza kuanza mafunzo ya mchezo wa kuogelea na kusoma katika shule ya St Felix.
Mugogeleaji wa Tanzania kutoka klabu ya Morogoro, (Mis Piranha) , Dennis Mhini ameondoka jana kwenda Uingereza kuanza mafunzo ya mchezo huo pamoja na masomo katika shule ya St Felix. Dennis aliagwa na familia yake ikiwa pamoja na baba, Hamis Mhini na Mama, Bhoke Mukoji kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Muogeleaji huyo ambaye amepata nafasi ya kusoma na kujifunza mchezo huo kupitia kipahji chake amesema kuwa atahakikisha anatumia fursa hiyo vizuri na kuiletea Tanzania medali ya kwanza kupitia mchezo wa kuogelea.
“Ndoto zangu zimetimia, leo (jana) ndiyo naamini kuwa kupitia kipiaji changu na bidi katika masomo, naenda Uingereza kwa ajili ya nia moja tu, kuongeza ujuzi na
Dennis aliyeiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki ya Vijana nchini, Argentina amepata nafasi hiyo baada ya kufikiwa viwango vilivyowekwa na shule hiyo chini ya kocha maarufu, Sue Purchase. Kigezo cha kwanza ni ubora wake katika mchezo kuogelea baada ya kufikia muda unaotakiwa na pili uwezo wake wa darasani.
Baba wa mchezaji huyo, Hamis Mhini alisema kuwa mwanaye pamoja na kutoweza kutwaa medali Argentina, alifanikiwa kupunguza muda wake wa kuogelea, jambo ambalo limewavutia sana walimu na kocha maarufu wa mchezo wa kuogelea nchini uingereza, Sue Purchase. Mhini alisema kuwa hatua hiyo ni kubwa katika maendeleo ya mchezo wa kuogelea nchini kwani anaamini kuwa mwanaye ataiva na kuwa muogeleaji bora Tanzania na dunia.
Alisema kuwa Dennis anapenda sana mchezo wa kuogelea na ndiyo maana waliamua kumpa nafasi ya kufanya kile ambacho anakipenda na kufikia kiwango cha kufuzu michezo ya Olimpiki ya Vijana iliyofanika mjini Buenos Aires.
Katika michezo hiyo, Dennis aliweza kushika nafasi ya tatu katika kundi la kwanza kweye staili ya freestyle ya mita 100 kwa kupata muda wa sekunde, 58.53 na pointi 514 na vile vile kumaliza katika nafasi ya tatu kwa upande staili ya backstroke kwa mita 50 kwa kutumia sekunde 29.79 na kupata pointi 525.
Dennis alisema kuwa amefurahi sana kupata nafasi hiyo na kuahidi kufanya mambo makubwa kwa Taifa lake.
Hivyo makala Mhini aenda kujiunga St Felix Uingereza, aahaidi kuleta medali ya kwanza ya kuogelea Tanzania
yaani makala yote Mhini aenda kujiunga St Felix Uingereza, aahaidi kuleta medali ya kwanza ya kuogelea Tanzania Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mhini aenda kujiunga St Felix Uingereza, aahaidi kuleta medali ya kwanza ya kuogelea Tanzania mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mhini-aenda-kujiunga-st-felix-uingereza.html
0 Response to "Mhini aenda kujiunga St Felix Uingereza, aahaidi kuleta medali ya kwanza ya kuogelea Tanzania"
Post a Comment