title : TRA WATANGAZA KIAMA WAFANYABIASHA WAKWEPA KODI KARIAKOO, WATOA SIKU SABA ZA MWISHO.
kiungo : TRA WATANGAZA KIAMA WAFANYABIASHA WAKWEPA KODI KARIAKOO, WATOA SIKU SABA ZA MWISHO.
TRA WATANGAZA KIAMA WAFANYABIASHA WAKWEPA KODI KARIAKOO, WATOA SIKU SABA ZA MWISHO.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA,) Mkoa wa Kikodi Kariakoo Warioba Kanire akizungumza na wafanyabiashara wa kariakoo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maduka yaliyofugwa na wafanyabiashara wa kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya wafanyabiashara hao kupata taarifa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanakagua matumizi ya mashine za kutoa risiti EFD.
Picha ya Duka la simu.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kikodi Kariakao imetoa muda wa siku saba wa kujirekebisha kwa wafanyabiashara wa Kariakoo ili wafate kanuni na taratibu wa kuuza bidhaa na kutoa risiti za mashine ya EFD kabla ya kupigwa faini.
Hatua hiyo imekuja baada ya TRA kuendelea kufanya ukaguzi duka hadi duka, huku wafanyabiashara wengine wakisema bado hawakuwa na elimu ya kutosha katika kufata taratibu za kufanya biashara.
Akizungumza na wafanyabiashara wa Karikaoo jijini Dar es Salaam wakati wa ukaguzi wa matumizi ya mashine za kutoa risiti EFD, Meneja wa TRA, Mkoa wa Kikodi Kariakoo Warioba Kanire, amesema kuwa baada ya muda wa siku saba kumalizika wafanyabiashara atakayebainika hatoi risiti atapigwa faini kuanzia ya milioni tatu.
Kanire amesema kuwa kuna wafanyabiashara wengi hawatumii mashine za kutoa risiti EFD baada ya kufanya mauzo kitu ambacho kinaikosesha serikali mapato.
"Wapo wafanyabiashara waminifu na wengine na sio waminifu, lakini wengine hawana elimu ila tayari tumewaelimisha, tutakapokuja tena tatawapiga faini wote ambao wanakwenda kinyume na sheria" amesema Kanire.
Ameeleza kuwa ni vizuri kila mtu akawa na mashine za EFD ili kuhakikisha kila mfanyabiashara analipa Kodi.
"Tumepita kufanya ukaguzi pamoja na kutoa elimu ili kuhakikisha wafanyabiashara wote wanakuwa na uwelewa wa kutosha" amesema Kanire.
Kanire ameeleza baada ya kufanya ukaguzi wafanyabiashara watafauta taratibu zote za TRA kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya taifa.
Hivyo makala TRA WATANGAZA KIAMA WAFANYABIASHA WAKWEPA KODI KARIAKOO, WATOA SIKU SABA ZA MWISHO.
yaani makala yote TRA WATANGAZA KIAMA WAFANYABIASHA WAKWEPA KODI KARIAKOO, WATOA SIKU SABA ZA MWISHO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TRA WATANGAZA KIAMA WAFANYABIASHA WAKWEPA KODI KARIAKOO, WATOA SIKU SABA ZA MWISHO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tra-watangaza-kiama-wafanyabiasha.html
0 Response to "TRA WATANGAZA KIAMA WAFANYABIASHA WAKWEPA KODI KARIAKOO, WATOA SIKU SABA ZA MWISHO."
Post a Comment