title : MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH.MILIONI TANO AU JELA MIAKA MITANO
kiungo : MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH.MILIONI TANO AU JELA MIAKA MITANO
MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH.MILIONI TANO AU JELA MIAKA MITANO
MFANYABIASHARA, Hafidhi Jonggradgorn amehukumiwa kulipa faini ya Sh. milioni tano au kutumikia kifungo cha miaka mitano gerezani baada ya kukiri kutenda makosa wawili likiwemo la kukutwa na madini ya Coloured Gemstones yenye usurp Wa kilogramu 67.76 na thamani ya USD 105.757.
Aidha Mahakama imeamuru madini hayo yataifishwe na wapewe Tume ya Madini.
Hukumu hiyo imesomwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Wakili wa Serikali, Jacqline Nyantori kumsomea mashtaka mshtakiwa huyo na alikiri makosa yote.
Akisomewa hati ya mashtaka, imedaiwa Kati ya Januari Mosi 2017 na June 3 mwaka huu maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, nchi za Falme za Kiharabu na India mshtakiwa akiwa si mtumishi wa umma kwa makusudi alifadhili biashara ya mchongo wa jinai kwa lengo la kujipatia faida.
Katika shtaka la pili, Wakili Nyantori amedai Juni 3 mwaka huu maeneo ya Mikocheni A mtaa wa Chwaku mshtakiwa huyo alikutwa na vito vya madini ya Coloured Gemstones Kilogramu 67.76 yenye thamani ya Dola za Marekani USD 105.757 bila ya kuwa na leseni na uhalali wa kuwa na madini hayo.
Kabla ya kusomewa hukumu hiyo Wakili Nyantori aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali itakayokuwa fundisho kwa wengine wanaofanya makosa kama hayo. Pia ameiomba Mahakama kutoa amri ya kutaifisha madini hayo kwa mujibu wa sheria na kuelekeza yawe chini ya Tume ya madini.
Katika utetezi wake, wakili wa Utetezi Habibu Mwenye anayemtetea mshtakiwa ameiomba Mahakama impunguzie adhabu mteja wake kwani anafamilia inamtegemea na kuwa Mtejatu wake huyo tangu alipoingia nchini mwaka 1989 hakuwahi kufikishwa Polisi wala mahakamani mpaka siku ambapo aliletwa kwa mashtaka hayo, hana rekodi ya uharifu.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mashauri alisema mshtakiwa anastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine hivyo katika shtaka la kwanza anamuhukumu kulipa faini ya Sh. Milioni mbili au jela miaka miwili na katika shtaka la pili anamuhukumu faini ya Sh. Milioni tatu au kwenda jela miaka mitatu.
Hakimu Mashauri amesema Mahakama pia imetoa amri ya kuyataifisha madini hayo na kuyapeleka Tume ya madini. Hata hivyo mshtakiwa huyo alilipa faini na kuachiwa huru.
Hivyo makala MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH.MILIONI TANO AU JELA MIAKA MITANO
yaani makala yote MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH.MILIONI TANO AU JELA MIAKA MITANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH.MILIONI TANO AU JELA MIAKA MITANO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mfanyabiashara-ahukumiwa-kulipa-faini.html
0 Response to "MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA SH.MILIONI TANO AU JELA MIAKA MITANO"
Post a Comment