title : DC MSAFIRI NIMERIDHISHWA NA USALAMA WA KIVUKO CHA MAGOGONI.
kiungo : DC MSAFIRI NIMERIDHISHWA NA USALAMA WA KIVUKO CHA MAGOGONI.
DC MSAFIRI NIMERIDHISHWA NA USALAMA WA KIVUKO CHA MAGOGONI.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Sarah Masafiri watatu kutoka upande wa Kulia wakwanza kulia ni katibu tawala wa kigamboni Rahel Mhando akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya alipo tembea kivuko cha Magogoni leo.(Picha na John Luhende )
Na. John Luhende
Mwamba wa habari.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe Sarah Msafiri, amefanya ziara katika Kivuko cha Magogoni kwaajili ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa majuma mawiliyaliyopita kwaajili ya kuboresha huduma na usalama wa Kivuko hicho.
Akizungumza katika ziara hiyo DC Msafiri, amesema ameridhidhishwa na utekelezaji wa maagizo yake ikiwemo suala la usalama wa Kivuko na kuu pongeza uongozi wa TEMESA kwa Maboresho hayo, na kusisitaza ufungazi wa Camera za usalama na namba ya simu ya dharula itayotumiwa na wananchi wanaopatahuduma wakati wa dharula.
“Nilitoa maagizo maagizo hapa wakati wa ziara yangu leo nimerudi na kamati yangu ya Wilaya ya ulinzi na usalama maagizo yamatekelezwa kwa kiasi kikubwa namba za simu za dharula wameweka namba za watendaji ,SUMATRA, OCD wa Polisi na zimamoto kwaajili ya kutoa taarifa , wana toa matangazo vizuri, na wanatoa elimu ya maokozi kwa njia ya Televisheni walizofunga ndani ya kivuko angalau elimu sasa inatolewa , na wameniahidi mwishoni mwezi huu wa kumi watafunga Camera za usalama , na nimefurahishwana namna walivyo panga maboya na wameyafasnyi usafi na hawafungitena kwa makufuli.” Amesema.
Pamoja na hayopia DC Msafiri ameagiza kubadilishwa kwa Tv ndogo zilizofunwa nadani ya kivuko zitolewe zifungwe nadani na zile kubwa zifungwe ndani ya kivuko, na amesema pia ameridhishwa na usafi ulifanywa kwa vifaa za uokozi ikiwemo maboya ambapo siku ya kwanza yalikuwa na vumbi ,Buibui na Mende.
Akizungumzia Wavuvi ameagiza mamlaka zinazohusika kukutana kujadili namna wavuvi wanavyo paswa ku kuengeza mitumbwi yao,na kupiga vita uvuvi haramu, na kuzuia mitumbwi kubeba na kusafirisha abiria.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji mkuu wa TEMESA Mhandisi Japhet Masele amesema, wametekeleza maagizo ya DC na kumshukuru ushirikiano wa kamati ya ulinzi na usalama na kusema kuwa baadhi ya maboya machache yalibakia wataendelea kuyatekeleza na kueleza kuwa TEMESA itaendelea kuboresha huduma za vivuko vyote nchi nzima na wataweka electronic counter ya kutambua idadi ya abiria wanaopatahuduma katika Kivuko.
“Aliyo yasema mkuu wa Wilaya tutayatekeleza na si hapatu bali nchinzima katika vivuko vyetu , na hapa kigamboni tuna fanya upanuzi wa sehemu ya kusubia abiria na lengo letu nikutoa huduma bora kwa wananchi” amesema
Hivyo makala DC MSAFIRI NIMERIDHISHWA NA USALAMA WA KIVUKO CHA MAGOGONI.
yaani makala yote DC MSAFIRI NIMERIDHISHWA NA USALAMA WA KIVUKO CHA MAGOGONI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MSAFIRI NIMERIDHISHWA NA USALAMA WA KIVUKO CHA MAGOGONI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/dc-msafiri-nimeridhishwa-na-usalama-wa.html
0 Response to "DC MSAFIRI NIMERIDHISHWA NA USALAMA WA KIVUKO CHA MAGOGONI."
Post a Comment