title : DC MJEMA AWABANA WATENDAJI NGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI.
kiungo : DC MJEMA AWABANA WATENDAJI NGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI.
DC MJEMA AWABANA WATENDAJI NGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI.
Na John Luhende
Mwamba wa habari
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewataka Watendaji, Wenyeviti, wa mitaa na wakuu wa Idara katika Manispaa ya Ilala kushughulikia kero zinazowakabili wananchi,ili kuleta maendeleo.

DC Mjema ameyasemahayo Leo alipokuwa akifanyamajumuisho ya Ziara yake alipotembelea kata zote za majimbo yote katika halimashauri hiyo na kueleza kuwa amesikiliza jumla ya kero 2265katika ziara hiyo, ambapo amefanya makubaliano nao kuhakikisha wanatenda kazi ipasavyo, na kuwaahidi kuwachukulia hatua watakao shindano kutatua kero za wanachi.

Amesema hataki kuona tena Kero hazitatuliwi katika ngazi za chini ambapo zinaweza kusikizwa na Mtendaji wa mtaa, Mwenyekiti wa mtaa, Mtendaji kata,au Afisa Tarafa.
"Ofisi yangu imekuwa ikipokea wananchi wanaowasilisha Kero zao ,Sasa Kero hizo zinakuwa hazipatiwi ufumbuzi na watendaji badala yake wananchi wanakimbilia kwa Mkuu wa Wilaya au wanasubiri Mkuu wa Wilaya awatembelee ili waeleze Kero zao jambo hili halikubaliki"Amesema Mjema.
Amesema lengo la Serikali za mitaa ni kusogeza huduma karibu na wananchi na Kila kiongozi katika ngazi mbalimbali aliyechaguliwa, kuteuliwa au kuajiriwa anapaswa kishughulika na matatizo ya wananchi.
Katika Ziara hiyo amesema zipo Kero zilizopata ufumbuzi papo kwa papo na nyingine zilizochukuliwa na kupelekwa katika ngazi husika ambapo Ni katika hataua mbalimbali za kutafutia Ufumbuzi.
Miongoni mwa migogoro iliyotatuliwa Ni Pamoja na Mgogoro wa eneo la Minjingu kata ya Pugu,ambapo Waziri wa Ardhi alikubali ombi la lutowaondoa wananchi katika eneo hilo., Mgogoro wa kuhifadhi Msitu Kazimzumbi, Mgogoro wa Upanuzi was uwanja was ndege Pamoja na migogoro mingine mingi iliyojitokeza katika kata mbalimbali.
Aidha katika Mgogoro wa Afya amataka wauguzi Pamoja na wafanyakazi katika sekta ya Afya wanaotumia lugha mbaya na chafu kwa wagonjwa kuacha tabia hiyo vinginevyo watachukukiwa Hatua.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jumanne Shauri amesema manispaa hiyo imejipanga kukusanya mapato zaidi na kuendeleza ujenzi wa madara katika shule ilikukabiliana na uhapungufu wa madarasa ilikuhakikisha wanafunzi wote walichaguliwa wanaenda shule huku akwapongeza walimu na wadau wa elimu wa manispaa hiy kwa kuwezeha wilaya hiyo kushika nafasi yanne kitaifa katika matokeo ya mtihani wa Darasa la saba mwaka huu.
Hivyo makala DC MJEMA AWABANA WATENDAJI NGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI.
yaani makala yote DC MJEMA AWABANA WATENDAJI NGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC MJEMA AWABANA WATENDAJI NGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/dc-mjema-awabana-watendaji-ngazi-za.html
0 Response to "DC MJEMA AWABANA WATENDAJI NGAZI ZA CHINI KUTATUA KERO ZA WANANCHI."
Post a Comment