CCTV CAMERA ZILIVYONASA TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI

CCTV CAMERA ZILIVYONASA TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa CCTV CAMERA ZILIVYONASA TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : CCTV CAMERA ZILIVYONASA TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI
kiungo : CCTV CAMERA ZILIVYONASA TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI

soma pia


CCTV CAMERA ZILIVYONASA TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI





Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ alitekwa jana alfajiri Oktoba 11, 2018 jijini Dar es Salaam kwenye Hoteli ya Colosseum iliyopo Oysterbay alipokwenda kwa lengo la kufanya mazoezi.

Akizungumzia tukio hilo jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema katika uchunguzi wao wa  awali kupitia kamera za ulinzi (CCTV) zimeonyesha magari mawili yalihusika.

Mambosasa amesema katika tukio hilo magari hayo mawili yalifika hotelini hapo kabla MO hajafika.

Amesema gari ya kwanza aina ya Toyota Surf ilikuwa imeegeshwa nje ya geti la kuingilia hotelini likiangalia usawa wa ndani ya hoteli, huku la pili aina ya Toyota Noah likiegeshwa pembeni kidogo ya eneo ambalo MO hupaki gari lake kila afikapo hotelini na kushuka.

Wakati Mo akifika hapo kamera zilionyesha gari ya ndani aina ya Noah ikiiwashia taa gari ya nje kuashiria kwamba Mo amefika.

Mara baada ya kuwasha taa hizo wakati Mo anashuka watu wawili raia wa kigeni (Wazungu) waliteremka na kuingia ndani ya geti la kuingilia kisha kukutana na Mo akiwa anafunga gari yake na kuanza kuingia ndani ya jengo.

Watu hao wawili walifika kwa Mo na kufanikiwa kumbana vizuri ambapo wakati wakiendelea na kazi hiyo gari iliyopaki nje ilikuwa imeshafanikiwa kuingia ndani ya geti na watekaji kufanikiwa kumuingiza katika gari iliyotoka nje aina ya Surf.

Mara baada ya watekaji kufanikiwa walimpokonya funguo ya gari na simu yake kisha kuzitupa chini na kuanza safari ya kuondoka eneo hilo.

Kamera zilionyesha tukio hilo lilikamilika majira ya saa 11:35 alfajiri ambapo wakati wanatoka, Surf ambayo ilimbeba Mo ilitangulia mbele huku Noah ikifuata nyuma mpaka kwenye geti la kutokea.

Walipofika hotelini hapo Wazungu hao, alishuka mmoja na kufyatua risasi mbili juu kuamrisha mlinzi afungue geti ambapo wakati walinzi wakijisalimisha Mzungu aliyeshuka akakimbia getini na kufungua geti mwenyewe na gari zote kufanikiwa kukimbia.


Hivyo makala CCTV CAMERA ZILIVYONASA TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI

yaani makala yote CCTV CAMERA ZILIVYONASA TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala CCTV CAMERA ZILIVYONASA TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/cctv-camera-zilivyonasa-tukio-la.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "CCTV CAMERA ZILIVYONASA TUKIO LA KUTEKWA MO DEWJI"

Post a Comment