WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA

WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA
kiungo : WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA

soma pia


WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea msaada wa dawa na vifaa tiba wenye thamani ya Sh.Bilioni mbili kutoka Serikali ya India.

Msaada huo wa dawa na vifaa tiba wa Serikali ya India umekabidhiwa kwa Waziri Mwalimu na Balozi wa India nchini Tanzania na kwamba dawa na vifaa tiba hivyo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ambayo imedhamiria kuboresha sekta ya afya.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada huo Waziri Mwalimu ameishukuru Serikali ya India kwa kutoa msaada huo ambao umetokana na ombi la Rais Dk.John Magufuli kwa Waziri Mkuu wa India ambaye alikuja nchini.

"Wakati Waziri Mkuu wa India alipokuja nchini,Rais Dk.John Magufuli alitoa ombi la kuomba dawa muhimu na vifaa tiba.Hivyo tunatoa shukrani kwa Serikali ya India kwa msaada huu.Tunatoa shukrani kwa Waziri Mkuu wa India," amesema Waziri Mwalimu.

Akizungumzia zaidi msaada huo,Waziri Mwalim amesema miongoni mwa dawa ambazo zimetolewa na Serikali ya India  ni dawa aina ya Amoxline kwa ajili ya watoto na zipo dozi 19800.
Pia kuna dawa ya kuzuia wajawazito kuvuja damu baada ya kujifungua na kwamba kuna dawa za chanjo ya homa ya ini.
 
Waziri Mwalim amesema kuwa dawa na vifaa tiba vitapelekwa kwenye Hospitali za umma na kwamba pamoja na msaada huo Serikali imefanikiwa kuboresha sekta ya afya ikiwemo ya kuongeza dawa na vifaa tiba.

"Dawa ambazo zimetolewa zitatolewa bure.Hii imedhihirisha mahusiano mazuri kati ya Tanzania na India.Kwa kukumbusha tu baada ya Rais Magufuli kuingia madarakani tumekuwa tukinunua dawa kutoka viwandani badala ya watu binafsi.

" Tunaomba Balozi wa India uendelee kuhamasisha wawekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba waliopo India kuja kuwekeza nchini kwa kujenga viwanda vya dawa,"amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Wakati huo huo Waziri Mwalimu amezungumzia namna ambavyo Serikali imefanikiwa kuongeza dawa muhimu nchini ambazo kwa sasa zipo za kutosha.

Amefafanua  kuwa taarifa ya Bohari ya Dawa nchini(MSD) ni kwamba kuna ongezeko kubwa la  dawa muhimu hadi  kufikia asilimia 85 kutoka asilimia 36 huko nyuma.

Pia amesema Serikali imeendelea kuhakikisha dawa zote zinakwenda katika maeneo yote ili wananchi wenye mahitaji ya dawa wazipate.

"Kati ua muhimu ya dawa ambazo zimepewa kipaumbele ni dawa ya kumuwezesha mama mjazito kutojifungua mtoto mwenye kichwa kikubwa na mgongo wazi," amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Kwa upande wake Balozi wa India nchini Tanzania Sandeep Arya amesema thamani ya msaada ambao umetolewa na Serikali yao una thamani ya Sh.bilioni mbili na lengo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuboresha sekta ya afya.
"Dawa na vifaa tiba hivyo unalenga kusaidia kuboresha sekta ya afya nchini Tanzania.Pia msaada huu unathibitisha ushirikiano na uhusiank mzuri kati Serikali hizi mbili," amesema Balozi Arya.


Hivyo makala WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA

yaani makala yote WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/waziri-ummy-mwalimu-apokea-msaada-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI UMMY MWALIMU APOKEA MSAADA WA DAWA,VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA INDIA"

Post a Comment