Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza

Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza
kiungo : Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza

soma pia


Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza

Watu  wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine wanane kujeruhiwa vibaya katika ajali ya mabasi mawili yakugongana uso kwa uso katika kijiji cha Kamanga, Sengerema mkoani Mwanza saa nne asubuhi jana.

Akizungumzia ajali hiyo, shuhuda aliyekuwa katika pikipiki na kunusurika kugongwa na mabasi hayo, Philipo Budeba, alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mabasi yote mawili.

“Mimi nilikuwa naendesha pikipiki, mbele yangu kulikuwa na basi la Mkombozi Trans lenye namba T540 DLF na nyuma kulikuwa na Basi la Walawi Express lenye namba T167 CSN yote yalikuwa na mwendokasi," alisema Budeba.

"Dereva wa Mkombozi ndiye aliyetaka kupita gari lingine, lakini ilishindikana na kusababisha magari hayo kuvaana... mimi nilijirusha kwenye kilima cha pembeni mwa barabara."

Naye abiria wa Mkombozi Trans iliyokuwa ikitokea Kanyara Buchosa, Sengerema, Fransisco Kansola alisema tabia ya madereva kushindwa kuchukua tahadhari na kujali kuwahi abiria ndiyo chanzo cha ajali hiyo.

Walawi Express lilikuwa likitoka Mwanza kwenda Nemba wilayani Biharamulo.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema dereva wa basi la Walawi, Frank Kimboka ni miongoni mwa majeruhi wanane wa ajali hiyo baada ya kujeruhiwa miguu yote.

“Waliofariki ni dereva wa basi la Mkombozi Trans aliyefahamika kwa jina la Simon Mdalesalamu na mwanamke aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20," alisema Kamanda Msangi.

Majeruhi watatu wametajwa kuwa ni Frank Mushi aliyevunjika miguu yote miwili, Isaack Hamisi (22) mkazi wa Nyasaka wilayani Ilemela na Mwinyi Ismail (50) aliyevunjika miguu yote miwili, alisema Kamanda Msangi.

"Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mabasi hayo.”

Aidha, ajali hiyo ilitokea wakati mkoa wa Mwanza ukizindua maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, yenye kaulimbiu inayosema ‘Zuia ajali, tii sheria, okoa maisha'.

Majeruhi walikimbizwa katika Hospitali ya Rufani ya Bugando jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu.


Hivyo makala Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza

yaani makala yote Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/ajali-ya-basi-yaua-wawili-na-kujeruhi-8.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Ajali ya Basi Yaua Wawili na Kujeruhi 8 Jijini Mwanza"

Post a Comment