WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA

WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA
kiungo : WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA

soma pia


WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA

NA TIGANYA VINCENT-RS TABORA
JUMLA ya watahiniwa 35,430 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi unaonza kesho mkoani Tabora.

Kauli hiyo imetolewa leo na Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Sussan Nusu wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake.

Alisema kuwa mtihani huo utakaofanyika kwa siku mbili mfululizo na kuongeza kuwa kati ya watahiniwa hao watoto wa kiume ni 16,706 na watoto wa kike ni 18,724.

Nusu alisema jumla ya watoto 34,762 ni kutoka shule Serikali za kawaida ambapo wanafunzi wa kiume ni 16,359 na wasichana 18,403 na wanafunzi kutoka shule zinazofundisha kwa lugha ya Kiingereza ni watoto 651.

Alisema jumla ya wanafunzi 17 wenye mahitaji maaluma ikiwa ni wenye uoni hafifu 10 na wasioona kabisa saba nao wanatarajia kufanya mtihani humo.

Afisa Elimu huyo wa Mkoa alisema maandalizi zoezi hilo yamekamilika na vifaa vyote muhimu vimeshafikishwa katika maeneo husika na wasimamizi wanatakiwa kupelekwa katika vituo walivyopangiwa.

Nusu aliwataka Wasimamizi wote Mkoani hapa kuwa makini na kuzingatia uaadilifu wakati wote wa usimamizi wa mitihani na kuongeza kuwa ni vema wazingatie maelekezo yote waliopewa wakati wa semina.

Kwa upande wa wazazi aliwataka kuhakikisha wanakaa na watoto wao na kuwapa maneneo ambayo yatawapa moyo ili waweze kufanya mitihani yao kwa kuniamini na kutumia mafunzo yote waliopatiwa

Alisema wazazi pia wanalo jukumu la kuhakikisha watoto wao wote waliosajiliwa kufanya mitihani isipokuwa kwa wale wenye kibali cha Daktari.

Nusu alisema kuwa hadi kufikia leo ni mtoto moja kutoka Urambo mkoani humo ambaye hataweza kufanya mitihani kwa sababu ni mgonjwa na Daktari amesema apumzike.

Kuhusu watoto aliwataka kujiamini kwani mtihani wanaoenda kufanya ni sawa na ile ambayo wamekuwa wakifanya kama vile ya utimilifu na inayoandaliwa na walimu wao.

Watoto wanaomaliza mwaka huu mkoani Tabora waliandikishwa kuanza Darasa la Kwanza mwaka 2012 wakiwa 41,789 ikiwa ni wavulana 21,898 na wasichana 19,600.


Hivyo makala WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA

yaani makala yote WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/watoto-35430-kufanya-mtihani-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WATOTO 35,430 KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MKOANI TABORA"

Post a Comment