title : SIKU YA MOYO DUNIANI YAADHIMISHWA KWA KUTOA ELIMU NA UPIMAJI WA AFYA
kiungo : SIKU YA MOYO DUNIANI YAADHIMISHWA KWA KUTOA ELIMU NA UPIMAJI WA AFYA
SIKU YA MOYO DUNIANI YAADHIMISHWA KWA KUTOA ELIMU NA UPIMAJI WA AFYA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
SIKU ya moyo duniani imeadhimishwa jana Septemba 29 ikiwa lengo mahususi kwa kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kujua na kupima magonjwa mbalimbali ya moyo, pamoja na kuelimisha jamii juu ya athari mbalimbali zinazotokana na magonjwa ya moyo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa afya, wazee, jinsia na watoto Faustine Ndugulile amesema kuwa maadhimisho ya Siku ya Magonjwa ya Moyo Duniani mwaka yamekuja na kauli mbiu ya ‘MOYO WANGU, MOYO WAKO’ kwa lugha ya kiingereza My heart, Your heart, ikiwa na lengo la kusisitiza juu ya kila mmoja wetu kufanya uchunguzi wa moyo ili kujua hali yake.
Aidha amesema; "Magonjwa ya moyo yanaongoza kwa kusababisha vifo duniani. Inakadiriwa kuwa watu 17,500,000 hufa kila mwaka duniani kote kutokana na magonjwa ya moyo na kiharusi. Ugonjwa wa moyo ni ugonjwa ambao unaathiri watu wa rika na jinsia zote; watoto, watu wazima, wake kwa waume. Aidha, Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaeleza kwamba asilimia 40% ya vifo vyote vinavyotokea duniani vinasababishwa na magonjwa ya moyo. Pia nusu ya vifo ambavyo vinatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza vinatokana na magonjwa ya moyo na vilevile asilimia 80% ya vifo hivi hutokea kwenye nchi zenye uchumi wa kati na wa kiwango cha chini" amesema Ndugulile.
Aidha imeelezwa kuwa matumizi ya tumbaku na bidhaa zake yanakadiriwa kusababisha vifo vya watu 6,000,000 duniani kila mwaka na pia huchangia kusababisha asilimia 10% ya wagonjwa wenye magonjwa ya moyo. Vilevile moshi wa sigara kwa watu wasiovuta sigara (second hand smoking) husababisha vifo vya watu laki sita (600,000) na kati ya hao 28% ni watoto. Hii ni kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani (WHO).
Pia amesema kuwa kama hatua madhubuti za kinga, uchunguzi wa mapema na tiba stahiki hazitachukuliwa haraka, tatizo la Moyo ifikapo mwaka 2035 litaongezeka na kufikia makadirio ya wagonjwa wapya milioni 131,978,870 (sawa na ongezeko la 45% kutoka hali ilivyo kwa sasa), huku ongezeko kubwa likiwa katika ukanda wa nchi zinazoendelea, Tanzania ikiwa moja wapo.
Matembezi ya Siku ya Moyo Duniani yakiendelea, ambayo kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu ya 'Moyo wangu, Moyo wako"
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongoza mazowezi siku ya Moyo Duniani yaliyoanzia viwanja vya Leaders Club na kumalizikia viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, matembezi hayo yalibeba kauli mbiu ya "Moyo wangu Moyo Wako". Wakwanza Julia ni Mkurugenzi wa kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Wizara ya Afya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile akikagua moja kati ya mabanda yaliyokuwepo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam,katika maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani. Kushoto kwake ni Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania Dkt. Robert Mvungi, kulia kwake ni Mkurugenzi wa kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Wizara ya Afya Dkt. Amalberga Kasangala
Madaktari wakitoa elimu na kupima afya za wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani.(picha na Emmanuel Massaka wa Global ya jamii).
Hivyo makala SIKU YA MOYO DUNIANI YAADHIMISHWA KWA KUTOA ELIMU NA UPIMAJI WA AFYA
yaani makala yote SIKU YA MOYO DUNIANI YAADHIMISHWA KWA KUTOA ELIMU NA UPIMAJI WA AFYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIKU YA MOYO DUNIANI YAADHIMISHWA KWA KUTOA ELIMU NA UPIMAJI WA AFYA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/siku-ya-moyo-duniani-yaadhimishwa-kwa.html
0 Response to "SIKU YA MOYO DUNIANI YAADHIMISHWA KWA KUTOA ELIMU NA UPIMAJI WA AFYA"
Post a Comment