Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa.

Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa.
kiungo : Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa.

soma pia


Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa.

 


 
 
Na Mwandishi Wetu
mwamba wa habari
Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza limeanza ziara
ya kutoa elimu juu ya ugonjwa huo katika mikoa ya Kanda
ya Ziwa.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Mradi wa Shirikisho hilo Happy
Nchimbi,ambapo amebainisha kuwa tayari wameanza kampeni inayolengo
kuvifikia vyuovya mbali mbali nchini na shule za msingi na sekondari
kuelimisha juu ya ugonjwa huo.

Amesema kuwa shinikizo la juu la damu ni kati ya magonjwa
yasiyokuwa ya kuambukizwa ambapo asilimia ya wagonjwa wa
ugonjwa huo haioneshi kupungua.

"Tumeanza kampeni hiyo katika mikoa ya kana ya ziwa ambapo
kuanzia septemba 20 na 21 tumetoa elimu juu ya magonjwa hayo
kwenye Chuo cha Walimu Shinyanga na kuwa zoezi la uelimishaji
limepokelewa vema,"amesema Happy.

Happy amesema kuwa zoezi hilo linaendelea septemba ambapo
Septemba 22 na 23 watakuwa Chuo cha Walimu Butimba mkoani
mwanza.


Amesema katika kuendelea na uelimishaji huo Kanda ya Ziwa Septemba
24 na 25 watakuwa Musoma Utalii Teachers and High School .

Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza limeanza ziara hiyo
ikiwa ni kuhakikisha vijana wanapata elimu ya kutosha ili kuweza
kuelimisha UMMA na familia zinazozingatia mitindo bora ya maisha
ikiwa pamoja na ulaji unaofaa na kufanya mazoezi na kuepuka
matumizi ya Sigara na unywaji wa pombe uliozidi.


Meneja huyo pia alisisitiza kuwa kwakuwa serikali ina mpango
wa kurekebisha mitaala ya elimu nchini Shirikisho hilo la Magonjwa
yasiyo ya Kuambukiza limeanza kampeni kutaka magonjwa yasiyo
yakuambukizwa kuingizwa katika mitaala.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa magonjwa yasiyo yakuambukizwa Profesa Andrew
Swai alisema kampeni waliyoianzisha ya kupima kwa hiari magonjwa ya
kuambukizwa iliyoamzia katika viunga vya Chuo Kikuu Huria Dar es Salaa
Salaam hivi karibuni alisema tatizo kubwa lipo katika ulaji usiofaa,kwakuwa watu
wamekiuka misingi ya ulaji usiofaa na badala yake hujilia kwa kadri wawezavyo
hivyo ameitaka jamii kuzingatia ulaji unaofaa.


Profesa Swai alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu za shirika la Afya duniani
za mwaka 2012 na tafiti zinazofanywa marakwamara na Shirikisho la Vyama vya
Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza, inaonesha shinikizo la juu la damu ni ugonjwa
unaongoza kuliko magonjwa yote yasiyo kuwa ya kuambukizwa.

Ripoti ya ya WHO ya 2012 inaonesha wagonjwa wanaougua plesha wanaongoza kwa
aslimia 26, sukari asilimia 9, na hata baada ya utafiti huo imeonekana ugonjwa
wa plesha umeongezeka mara tatu kuanzia 2012.


Imeelezwa kuwa watu 9 kwa kila 100 ya Watanzania wenye umri wa miaka 25
na kuendele wana ugonjwa wa kisukari,hata hivyo inatajwa kuwa kati ya
hao 9 ni wawili tu wanaojijua kuwa wanakisukari.


Hivyo makala Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa.

yaani makala yote Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/shirikisho-la-magonjwa-yasio-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Shirikisho la magonjwa yasio ya kuambukiza laanza ziara Kanda ya Ziwa."

Post a Comment