title : SERIKALI KUPAMBANA NA MIMEA VAMIZI NGORONGORO
kiungo : SERIKALI KUPAMBANA NA MIMEA VAMIZI NGORONGORO
SERIKALI KUPAMBANA NA MIMEA VAMIZI NGORONGORO
Serikali imeazimia kurudisha ikolojia ya hifadhi ya Ngorongoro katika mazingira yake ya asili na kusisitiza kuwa shughuli zote za kuharibu na kuchafua ikolojia hiyo vitadhibitiwa kwa nguvu na uwezo wote.
Akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba amesema kuwa lengo la ziara yake ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwa Mamlaka hiyo mwezi Machi 2017.
Katika ziara yake mapema mwaka jana pamoja na mambo mengine Waziri Makamba aliagiza Mamlaka hiyo kuchukua hatua za haraka na kuwaelekeza wamiliki wa hoteli na loji hususan zilizoko katika kingo za kreta katika bonde la Ngorongoro kutafuta vyanzo mbadala vya maji na kuondokana na kutegemea chanzo cha chemichemi za Lerai.
Aidha, Waziri Makamba aliagiza kuchukuliwa kwa hatua za haraka ili kudhibiti mimea inayohatarisha uoto wa asili katika Mamlaka ya Ngorongoro kwa kuunda jopo la wataalamu kutoka Tume ya Sayansi na Tecknolojia, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Hifadhi za Taifa za Tanzania, Wizara ya Kilimo na Mifugo na Mamlaka ya Ngorongoro ili kufanya utafiti wa kina na wakisayansi wa kubaini mbinu mpya ya kupambana na mimea hiyo vamizi inayotawala mimea inayotumiwa na wanyama kama malisho.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa maagizo hayo Kaimu Mhifadhi wa Ngorongoro Dkt. Maurus Msuha amesema kuwa Mamlaka ya Ngorongoro iliwaandikia barua wamiliki wote wa hoteli na loji na kufanya tafiti kupitia kwa wataalamu elekezi wawili tofauti ambao kwa pamoja walishauri kuandaliwa kwa mkakati wa usimamizi na matumizi ya maji ndani ya Mamlaka ya Ngorongoro utakaokuwa suluhisho la matatizo la maji bila kuathiri mifumo ya ikolojia katika Hifadhi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akiwa katika kikao na wadau na wamiliki wa hoteli zilizopo katika kingo za kreta katika bonde la Ngorongoro. Pamoja na mambo mengine Waziri Makamba amewata kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ya kutibu maji taka ili yaweze kutumika tena na kuwataka kufahamu kwa matumizi ya maji kutoka ndani ya kreta hitimisho lake linakaribia, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba akipata maelezo ya kitaalamu kutoka kwa Dkt. Linus Munishi mtafiti kutoka Taasisi ya Nelson Mandela. Taasisi hiyo imetenga eneo maalumu la majaribio ya kuua mimea vamizi bila kuathiri mazingira, utafiti unao onekana kufanikiwa.
Pichani ni mmea vamizi ambao unaathiri sana malisho ya wanyama katika bonde la Ngorongoro kreta. Serikali inachuka hatua za haraka kudhibiti mmea huo unaosambaa kwa kasi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SERIKALI KUPAMBANA NA MIMEA VAMIZI NGORONGORO
yaani makala yote SERIKALI KUPAMBANA NA MIMEA VAMIZI NGORONGORO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUPAMBANA NA MIMEA VAMIZI NGORONGORO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/serikali-kupambana-na-mimea-vamizi.html
0 Response to "SERIKALI KUPAMBANA NA MIMEA VAMIZI NGORONGORO"
Post a Comment