title : BARABARA YA MASWA-BARIADI KUONGEZA UKUAJI WA UCHUMI KANDA YA ZIWA
kiungo : BARABARA YA MASWA-BARIADI KUONGEZA UKUAJI WA UCHUMI KANDA YA ZIWA
BARABARA YA MASWA-BARIADI KUONGEZA UKUAJI WA UCHUMI KANDA YA ZIWA
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7 kwa kiwango cha lami, Mkoani humo.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu Mhandisi Albert Kent, akimuoesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, nyumba za Mhandisi Mshauri zilizojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya CHICO katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7 kwa kiwango cha lami, mkoani humo.
Muonekano wa kazi za ujenzi zikiendelea kwenye daraja la mto Simiyu katika barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa KM 49.7, Mkoani Simiyu
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
UJENZI unaondelea wa barabara ya Maswa-Bariadi yenye urefu wa Km 49.7 kwa kiwango cha lami unatarajiwa kufungua mkoa wa Simiyu na mikoa jirani ya Mara, Mwanza na Shinyanga hivyo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe mkoani Simiyu wakati akikagua barabara hiyo inayojengwa na mkandarasi wa kampuni ya CHICO na kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika ujenzi huo toka ulipoanza mwezi Oktoba mwaka 2017.
"Nimeridhishwa na hatua zilizofikiwa na nina imani mkandarasi atamaliza mapema mradi huu",amesisitiza Waziri Kamwelwe.
Aidha, ameupongeza uongozi wa mkoa huo na Wakala wa Barabara (TANROADS), kwa kusimamia mradi huo usiku na mchana na kuwataka kutoa taarifa muda wowote endapo kutakuwa na changamoto zinazoweza kukwamisha mradi huo.
Akizungumzia kuhusu Kiwanja cha Ndege cha Simiyu, Mhandisi Kamwelwe amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa hatua za awali zinaendelea katika kuhakikisha kiwanja hicho kinajengwa ili kufungua mkoa huo katika sekta za usafirishaji na uwekezaji.
Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Hivyo makala BARABARA YA MASWA-BARIADI KUONGEZA UKUAJI WA UCHUMI KANDA YA ZIWA
yaani makala yote BARABARA YA MASWA-BARIADI KUONGEZA UKUAJI WA UCHUMI KANDA YA ZIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BARABARA YA MASWA-BARIADI KUONGEZA UKUAJI WA UCHUMI KANDA YA ZIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/barabara-ya-maswa-bariadi-kuongeza_3.html
0 Response to "BARABARA YA MASWA-BARIADI KUONGEZA UKUAJI WA UCHUMI KANDA YA ZIWA"
Post a Comment