title : Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Castico Azindua Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Zanzibar.
kiungo : Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Castico Azindua Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Zanzibar.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Castico Azindua Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Zanzibar.
Na.Mwashungi Tahir-Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wanawake na Watoto Maudline
Cyrus Castico amezindua Mabaraza ya Wazee ambapo kwa
kuanzia Mabaraza hayo yatafanya kazi katika Jimbo la
Magomeni.
Kuundwa kwa mabaraza hayo kunakusudiwa kuwaweka
pamoja Wazee hao na kuanzishiwa miradi ya ujasiri amali ya
kuendeleza maisha yao na kuondokana na umasikini.
Akizindua Mabaraza hayo katika uwanja wa Meya Waziri
Castico ameitaka Jamii Wazee ipasavyo na kuheshimu
mawazo yao kwani ndio hazina kubwa kwa Familia na Taifa
kwa ujumla.
Amefahamisha kuwa Wazee wana haki ya kutoa mawazo yao
na kusikilizwa kutokana na kujua vitu vingi na uzoefu
unaotokana na umri mkubwa na utumishi wao.
Waziri Kastiko amesema Wazee hao wametumika muda
mwingi katika kazi mbalimbali Sekta binafsi na Serikali
ikiwemo Uhasibu na Nyanja mbalimbali za ulinzi hivyo
mawazo yao ni muhimu.
Aliongeza kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein amewapa kipaumbele
katika Serikali yake na huwapa pencheni ya kila mwezi ili
kujikimu mahitaji yao bila ubaguzi.
Amesisitiza kuwa Wizara yake iko makini katika kuhakikisha
wazee wote wanakuwa na mazingira mazuri ya kuwapatiwa
mambo muhimu yanayohitajika ikiwemo matunzo ya
uhakika na malezi bora.
“Wizara yangu iko mstari wa mbele kwa kuwalinda wazee
kwani wao ndio wenye fikira na busara katika kupanga
mambo ya maendeleo yao” .Alisema Waziri huyo.
Hata hivyo aliwasihi wazee hao kuzidisha mashirikiano na
kusaidia kuweka mikakati ya kupambana na vitendo vya
udhalilishaji ambavyo vimekithiri katika jamii.
Sambamba na hayo viongozi wa jimbo hilo akiwemo mbunge
Jamal Kassim Ali na Mwakilishi Rashid Makame Shamsi
wameahidi kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wazee hao na
kuwapatia huduma za afya.
Viongozi hao pia wameahidi kuwa karibu nao na kupokea
fikra na busara zao kwa kwa faida yao na Jimbo kwa ujumla.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
Hivyo makala Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Castico Azindua Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Zanzibar.
yaani makala yote Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Castico Azindua Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Zanzibar. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Castico Azindua Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Zanzibar. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/waziri-wa-kazi-uwezeshaji-wazee.html
0 Response to "Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Castico Azindua Baraza la Wazee Jimbo la Magomeni Zanzibar."
Post a Comment